Sunday, September 11, 2011

RingTone Kuingia kwenye SiasaAlex Nyanchoga-Ringtone

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Kenya Alex Nyanchoga Apoko maarufu kama Ringtone toka Kenya amefunguka kuwa ana mpango wa kuingia kwenye siasa na kwa sasa anakitolea macho kiti cha ubunge cha Kitutu Masaba

Ringtone atapigana kikumbo na Mwenyekiti wa ODM,Timothy Bosire kugombea ubunge baada ya Mbunge aliyeenguliwa na mahakama,Bw Walter Nyambati kuliacha wazi jimbo hilo la Kitutu Masaba na kwa sasa Ringtone anasubiri tarehe ya uchaguzi tu itangazwe na aanze harakati za kugombea ubunge huo.

Wanamuziki wa injili nchini Tanzania kutoka kushoto ni David Robert,Victor Mlahagwa,Bahati Bukuku, Addo November pamoja na Ambwene Mwasongwe.
Nchini Tanzania Mwanamunizi wa Injili Addo November ndiye mwanamuziki pekee wa Injili aliyeonyesha Nia ya kugombea ubunge.Addo au Baba Tuli katika uchaguzi uliopita alichukua fomu za kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha mapinduzi(ccm) lakini kura hazikutosha.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...