Kisima Award ni Tuzo za Muziki
zinazohoshimika sana nchini Kenya, Tuzo hizo huusisha muziki wa aina mbalimbali
kwa maana ya muziki wa kumtukuza Mungu pamoja na muziki wa Dunia(Circular
Music).
Katika Tuzo hizo za Kisima kwa Mwaka Huu
wa 2011 katika kategori ya Gospel Music ambayo imeunganisha wanamuziki wa injili
wa-kiume na wa kike pamoja na makundi na kuwa kategori moja. waliochaguliwa
kuwania Tuzo hiyo ni kama ifuatavyo.
GOSPEL – ARTIST GROUP OF THE YEAR
• Uwezo - Adonage
• I live for you - BMF
• Tobina - Daddy Owen
• Taunet Nelel - Emmy Kosgei
• Bahasha ya Ocampo - Juliani
• Papa God Oh - MOG/Mr Seed
Rappa Juliani |
Emmy Kosgei |
Mvutano mkubwa katika kategori hii ni
baina ya Mwanadada Emmy Kosgei ambaye ndiye Mwanamuziki Bora wa Kike barani
Afrika(Kwa mujibu wa Africa Gospel Music Awards 2011) pamoja na Rappa Julianni,
Juliani kwa sasa anaaminika kuwa ndiye Mfalme wa Gospel HipHop nchini humo.Juliani
kwa sasa anafanya Vizuri na Nyimbo yake iitwayo Barua ya Ocampo
aliyomshirikisha mwanadada Jaya.
Tofauti na Emmy na Juliani yupo pia Daddy
Owen, huyu anakubalika sana nchini humo na ndiye Mwanamuziki Bora wa Muziki wa
Injili Afrika mashariki(kwa mujibu wa AGMA 2011), nafasi ambayo ilikuwa
ikiwaniwa na Christina Shusho wa Tanzania.Daddy Owen ndiye mwanamuziki Bora Wa
Kiume nchini humo na hii ni kwa mujibu wa Groove Awards 2011.
Daddy Owen |
Nchini kenya kuna kuna tuzo nyingi za
Muziki ukilinganisha na hapa kwetu Tanzania ambapo tuna Tanzania Music Awards
pamoja na Tanzania Gospel Music Awards pekee. Kwa Upande wa Tuzo za Muziki wa
Injili nchini Kenya, Tuzo za Groove Awards ndizo zinazoheshimika sana nchini Humo.
No comments:
Post a Comment