Monday, September 5, 2011

John Lissu Aanza Jehova Yu Hai Tour


Mtumishi wa Mungu na Mwanamuziki mahiri wa nymbo za kusifu na kuabudu nchini aitwaye John Lissu jumapii ya jana amefanikiwa kuzindua rasmi ziara maalumu ya kusifu na kuabudu ijulikanayo kama JEHOVA YU HAI TOUR. Katika ibada hiyo Lissu huku alisindikizwa na makundi mbalimbali ya Injili kama Door keepers, Mch Maximilian Machumu, Upendo Nkone, Pastor Safari pamoja na Jackson Bentty kutoka Arusha,Lissu aliwaongoza watu katika sifa na kuabudu.

Kwa Mujibu wa Timu iliyoandaa tukio hilo, baada ya ziara hiyo kumalizika jijini Dar es salaam, Mtumishi wa Mungu John Lissu atazunguka Mikoani kwa ajili ya kumtukuza  Mungu. 

Watu wengi walijitokeza katika Ibada hiyo ya kusifu na kuabudu ilihali jiji la Dar es salaam siku ya jana likiwa na matukio mengi yanayohusu mwili wa kristo, moja kati ya matukio hayo ni pamoja na kuanza kwa Semina ya Mwl C. Mwakasege katika Viwanja vya Biafra huku katika Hotel ya Lamada kulikuwa na Tamasha lingine la Muziki wa Injili ambapo mwanamuziki Sarah K kutoka Kenya alikuwa akihudumu.

Jehova Yu Hai Tour


John Lissu akimtambulisha mkewe Nellis siku ya jana
John Lissu na Mkewe Nellis wakifanyiwa maombi kwa ajili ya huduma ambayo Mungu ameiweka ndani yao

John Lissu akiimba siku ya Jana

Umati wa watu uliojitokeza kuhudhuria ibada hiyo ya kusifu na kuabudu

Picha kwa Hisani ya SamPapaa

1 comment:

  1. good, watu wote wamenigusa, Mgisa na wengine Mungu afanye muujiza wa pekee kwenu, mmekuwa kiooo, Mgisa umefundisha mengi, watu hwajui namna sahihi ya kuachilia baraka za bwana, sijui nifanyeje wanunue cd zako alafu wamwone YESU live kupitia wewe, UA GREEEEEEET, BLESSED

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...