Wednesday, September 14, 2011

Mzee Maruge aliyejiunga Darasa la kwanza akiwa na Miaka 84


Mzee Maruge
Mwaka 2003 Mzee Maruge kutoka nchini Kenya akiwa na umri wa miaka themanini na Nne(84) aliamua kwenda kujiunga Darasa la kwanza nchini humo kitendo ambacho kiliuacha ulimwengu mzima hoi. Mzee huyo ambaye hadi kufikia umri huo hakujua kusoma wala kuandika alijitoa mhanga na kuamua kukaa darasani na VITUKUU vyake na wakawa ndio class mate wake.

Katika maisha ya wokovu kila siku tunaanza kujifunza kitu kipya katika Mungu kwa kuwa Mungu ni mpana kuliko Tunavyofikiri. Unaweza kuwa Muimbaji mzuri na ukasifika lakini kwenye eneo la kufundisha ukapwaya, na hivyo ukahitaji kuanza upya kujifunza juu ya hilo. Vile vile unaweza kuwa muombaji mzuri kwa vigezo vyako lakini Mungu kuna namna ya uombaji ambayo hakuna mwanadamu aliwahi kuifikia hivyo yahitaji ukae darasani na Mungu akufundishe kwa upya juu ya kuomba kwa viwango vya juu zaidi, na hivyo hakuna gradution ya 100% juu ya maarifa ya Mungu.

Siku zote Mungu  hutupa ufahamu wake kwa sehemu na kadri tuonyeshavyo bidii mbele zake hujifunua kwetu kwa sehemu.
Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...