Tuesday, September 13, 2011

Watangazaji wa Kubamba Tv Show Wapata Ajali


John Celeb
Baada ya majuma takribani mawili tangu watangazaji Silasi Mbise wa Wapo Fm,na Erick Brighton wa Praise Power radio  kupata ajali walipokuwa njiani wakitokea Morogoro wakirudi Dar es salaaam. Mwishoni mwa wiki iliyopita watangazaji pamoja na Ma Dj wa Gospel Music wa kundi la K-Crew la nchini KENYA nao walipata ajali siku ya alhamisi ya tarehe 8/09/2011.

Kwa mujibu wa Dj John Celeb anayefanya Video Mixing katika kipindi cha Kubamba Show kinachoendeshwa kila siku asubuhi na CITIZEN TELEVISION alisema ajali hiyo ilitokea katika kitongoji maarufu cha kakamega jijini Nairobi wakati wakiwa njian wakielekea kuhudumu Neno la Mungu katika shule za Sekondari. 

Baada ya ajali hiyo kutokea majeruhi wote walipelekwa katika Hospitali ya Agha Khan na kwa mujibu wa Celeb majeruhi wote kwa msaada wa Mungu wanaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...