Tuesday, September 6, 2011

Kutana na Jabu Hlongwane mmoja wa waanzilishi wa kundi la Joyous Celebration



Jabu Hlongwane sio jina geni kwa wafuatiliaji wa Muziki wa Injili barani Afrika, amezaliwa na kukulia katika nchi ya Afrika ya Kusini na ni miongoni mwa waanzilishi wa kundi maarufu Duniani la Kusifu na kuabudu liitwalo JOYOUS CELEBRATION lenye makazi yake nchini Afrika ya kusini. Waanzilishi wengine ni  Hlongwane, Mthunzi Namba pamoja na Lindelani Mkhize. 

Jabu Hlongwane
Jabu alizaliwa zaidi ya miaka 46 iliyopita na alifanikiwa kupata shahada ya ya sayansi ya mawasiliano(Communication Science). Baada ya kuhitimu Jabu alifundisha High Level somo la Lugha ya kiingereza kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kubahatika kupata offer ya kufundisha katika chuo kimoja nchini humo. 

Akiwa kama lecturer katika chuo hicho alikuwa akifanya vitu viwili kwa mpigo, alikuwa akifundisha na huku akiendeleza huduma yake ya uimbaji. Jabu aliendelea kufanya vitu hivyo vyote viwili kwa takribani miaka tisa kabla hajaamua kuachana na kufundisha na kuingia rasmi kwenye huduma ya uimbaji mnamo mwaka 1999.

Jabu Hlongwane akiwa na mmoja wa waanzilishi wa Joyous aitwaye Lindelani Mkhize, Mkhize awapo jukwaani huwa na makeke mengi na mara nyingi hupendelea kuvaa kofia

Baada ya kuingia kwenye huduma rasmi Jabu amekuwa Baraka kwa bara zima la Afrika na maekuwa akiiitwa sehemu mbali mbali nje na ndani ya Afrika  katika huduma yake ya uimbaji wa nyimbo za injili. Jabu, tofauti na uimbaji ni Mtunzi na mtayarishaji wa muziki(Producer) mpaka sasa amekwisha rekodi album zake binafsi zipatazo saba naya saba aliirekodi LIVE kwenye Dvd pamoja na Cd. Tofauti na album zake binafsi Jabu ameweza kutengeneza na kushiriki katika kutengeneza album za nyimbo za injili zaidi ya kumi na nane(18).

Kundi la Joyous Celebration
Jabu ambaye ni baba wa watoto wanne kwa mke wake mpenzi aitwaye Sibongile ambaye walikutana kwa mara ya kwanza wakiwa chuo kikuu zaidi ya miaka kumi na Tano(15) iliyopita. Miongoni mwa matukio ambayo Jabu anayakumbuka ni pale alipopata nafasi ya kuimba wimbo alioutunga uliohusu mambo ya katiba na aliuimba ndani ya Bunge la nchi hiyo ya Afrika ya kusini(RSA) siku ambayo katiba mpya ya nchi hiyo ilikuwa inazinduliwa.

Mnamo mwezi wa sita mwaka huu kutokana na sababu za ndani za kundi la Joyous, kundi hilo lilifanya usaaili wa watu wote wenye vipaji na wenye nia ya kujiunga na kundi hilo. Kwa mujibu wa Jabu watu wote walioonekana wanavipaji mbalimbali vya uimbaji na upigaji wa vyombo waliingia kwenye DATA BASE ya kundi hilo na pale ambapo kundi hilo litaonekana linauhitaji wa nafasi Fulani iwe ya uimbaji au upigaji walio kwenye database ndio wataitwa kwanza kuziba pengo hilo.
Album mpya ya Joyous Celebration iitwayo My Gift To You (  Joyous Cerebration 15) iliyozinduliwa mwezi wa nne mwaka huu wa 2011 ambayo ina Part 1 na 2

Kwa mujibu wa maelezo ya Jabu anasema pale ambapo wanakutana na mtu anakipaji kikubwa mno na wakalithibitisha hilo wao wanakuwa hawana jinsi zaidi ya kumuingiza mhusika moja kwa moja kwenye kundi hilo. Utararibu huu ndio uliopelekea wao walipokutana na Mnaigeria Uchechukwu(UCHE) wakaamua kumuingiza moja kwa moja kwenye kundi la Joyous Celebration.

Jabu akienda sawa stejini na Sipho Makhabane, Jabu alimshirikisha Sipho katika wimbo wake uitwao There is a Race (Keep Me True) uliomo katika album ya Jabu iitwayo Keep Me True

Jabu aliendelea kuwaambia waandishi wa habari kuwa, kwa sasa kundi linatafuta watu wenye vipaji tofauti na vilivyopo ndani ya kundi. Kifupi wanatafuta ladha mpya na kwa yeyote anayeimba sawasawa na waliopo kwenye kundi nafasi yake ya kuingia kundini ni ndogo, na kinachotafutwa ni kitu kipya ndani ya kundi.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...