Thursday, September 22, 2011

Aya Tatu: Ni Mungu pekee awezaye kutuchukulia mizigo yetu kila siku pasipo kuchoka
Zab 68:19 Na ahimidiwe Bwana siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu,    Mungu ndiye Mwokozi wetu.

Katika maisha yetu ya kila siku kuna tatizo moja kubwa, Mara tujalibiwapo tunatumia mno akili zetu na msaada toka kwa watu wanaotuzunguka ili kuondokana na tatizo hilo. Ni kweli Mungu hutumia akili zetu na watu waliokaribu nasi kutatua matatizo yetu, pamoja na hayo yote ni Lazima tufahamu kuwa ufumbuzi utokao kwa Mungu na sio kwa mwanadamu juu ya hali tunayopitia kila siku ndio wenye kudumu na usiokuwa na majuto ndani yake.

Tuingiapo katika jaribu kwanza yatupasa tujipange katika Mungu juu ya hilo tatizo pasipo kutegemea akili zetu na na jamaa wanaotuzunguka(Network) ili  yeye Mungu ndiyo afanye mlango wa kutokea . Tutegemeapo akili zetu kutatua tatizo  hutupelekea kuwa kama unabahatisha na huku ukijiuliza maswali Je ntafanikiwa au sitafanikiwa!!!!.Ukifikia hapo jua ndio umeikaribisha Hofu, na mara nyingi Hofu katikati ya jaribu hupelekea kufeli kabla hata hatujaanza kukabiliana na jaribu hilo, kwa kuwa HOFU haitokani na Mungu.

Ni Mungu pekee awezaye kutuchukulia mizigo yetu kila siku pasipo kuchoka, watu wengi hasa waliookoka  hulitambua hili, lakini pasipo kujijua au ni mazoea husubiri mpaka tatizo limekuwa sugu ndipo hurudi kwa Mungu kutafuta msaada kitu ambacho si sahihi. Yatupasa tumshirikisha Mungu kwanza katika kila hatua ya maishani na kuifanya Biblia kama Manual Book na Dira ya Maisha yetu yote chini ya Jua.

Mboya V.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...