Friday, September 23, 2011

Album Preview: Nakuabudu Bwana ya Josephine(Minza) Nkilla


Moja kati ya Video album za injili ambayo imekuwa chachu katika kumtukuza Mungu na kufanikiwa kufanya Vizuri sokoni ni pamoja Video album ya mwanadada Josephine Minza Nkilla iitwayo "NAKUABUDU BWANA". Sehemu kubwa ya Album hii ni kwa ajili ya Kumwabudu Mungu, Wale wapendao kumwabudu Mungu Tafuta album hii.Yafuatayo ni Mapitio ya album hii kuweza japo kwa sehemu nini hasa konachopatikana humo ndani.

Josephine Minza Nkila

Nimesogea Nikuabudu
Hii ni nyimbo ya kuabudu ambayo imefanyika Madhabahuni (stejini) kuanzia Mwanzo wa wimbo mpaka Mwisho. katika Nyimbo hii Minza amelead nyimbo nzima huku akiwa na takribani watu nane wakimback up. Nyimbo hii haina maneno mengi na muda mwingi timu nzima inaonekana ikiwa imezama ikimwabudu Mungu ikiimba “Nakwabudu Nakwabudu”. Katika Video hii Minza anaonekana akiwa amevaa koti la suti refu jeupe huku timu nzima ikiwa imevalia suti Nyeusi.

Minza akimwabudu Bwana katika Wimbo Nimesogea Nikuabudu

Timu nzima ikiwa uweponi katika wimbo Nimesogea Nikuabudu


Nakuabudu Bwana
“Nakuabudu Bwana, Nakutukuza Bwana , Nakuinua Bwana Unastahili” Haya ni maneno yanayoujaza wimbo huu wa Kuabudu. Katika Video hii kuanzia Mwanzo mpaka mwisho imefanyikia Madhabahuni huku akipata back up ya kutosha kutoka kwa watumishi wa Mungu. 

Moja kati ya Vitu vya msingi katika Video hii ni uwezo wa timu aliyonayo. Timu nzima inayomback-up inaonekana  iko serious na inajua inachokifanya Mbele za Mungu. Jamaa aliyefanya Video(Danny Kisuu)  amepiga Close up shoots nyingi na Long shoots kadhaa huku effects za stage Lights zimetumika kuinakshi Video.

Nakwabudu Nakwabudu Nakwabudu

Minza akilead nyimbo ya Nakwabudu Bwana
Roho Yangu Ikuimbie
Hii ni nyimbo Maarufu sana ya Tenzi Bwana Mungu Nashangaa, humo ndani Minza anaonekana akiabudu huku akiwa katika Location Tofauti tofauti zenye uoto wa Asili na zenye kupendea.Kuna mahali anaonekana yuko msituni na kuna mahali anaimba akiwa pembezoni mwa mto.Wakati ubeti wa Nikitembea unavyonza, Beat(ala) ya nyimbo hii inabadilika kutoka kuwa ya taratibu na kisha inakuwa a bit faster(inachangamka). 

Pindi nyimbo Inapochangamka na Minza Mwenyewe anaonekna akiuimba ubeti huu na kisha Chorous kwa furaha. Wakati Ubeti wa  YESU MWOKOZI  unapoanza, Beats(ala) zinabadilika tena na kurudi za taratibu . Tofauti nya nyimbo nyingine katika Video ya wimbo huu Minza Mwanzo mpaka Mwisho anaonekana akiwa peke yake akimsifu Mungu. Hii ni moja kati ya nyimbo zishushazo uwepo pindi ukiitazama.

Roho Yangu Na Ikuimbie, Jinsi wewe Ulivyo Mkuu

Jina Lako Mwokozi
Katika video hii Minza amemshirikisha mkaka mmoja ambaye ameweka Male vocal ya kutosha humo ndani, hii ni nyimbo ya taratibu ambapo Minza anaonekana akiimba na kucheza tartibu katika mandhali iliyotulia. Hahaaaaaa Humo ndani Minza katupia Mitupio ang`avu,  amevaa kimdada  na meshine vilivyo. Ala  ya nyimbo hii ni kama ya kiasili huku cameraman akipiga Long Shoots nyingi za ukweli.

Josephine Minza akiimba wimbo wa Jina Lako Mwokozi

Minza katika Jina lako Mwokozi

Ni wewe tu mtakatifu
Hii ni moja kati ya mfululizo wa nyimbo za kuabudu zilizomo ndani ya album hii, katika nyimbo hii Minza anasisitiza Ni wewe tu MTAKATIFU. Humo ndani kuna mdada anacheza mithili ya Yoga ambayo ni aina ya uchezaji jukwaani unaotumiwa sana na watumishi wa Mugu(waimbaji) katika nchi za Magharibi. Minza anaonekana akiwa kwenye koti refu jeupe huku timu inayomback  ikiwa ndani ya Suti nyeusi. Video ya Nyimbo hii Mwanzo mpaka Mwisho imefanyikia stejini.

Minza akiimba wewe ni mtakatifu kushoto ni binti akienda Sambamba na ala za wimbo huo

Inanipasa Kukusifu
Hii ni nyimbo pekee ya kusifu iliyoko ndani ya Album hii, Kuna lines zinasema ”Kila mwenye Pumzi ya Mungu amsifu Bwana maana kusifu kunawapasa wanyofu wa Moyo”. Kama wewe ni mpenzi wa sebene itafute hii nyimbo. Humo ndani wamo wakaka  wanaenda sambamba la beats wakicheza. Ndani ya nyimbo hii Minza amewashirikisha Emma na Danny amabao wote watatu Kwa  pamoja wameshirikiana Vizuri. 

Inanipasa Nikusifu

Raha ya Sebene sio tu kuimba ni pamoja na kucheza, hapa Minza Akisebeneka

AMEN AMEN HALELUYA
Amen Amen Haleluya  ni Bonus Track katika Video Album hii, Wimbo huu ambao ni AUDIO umesimama kama OUTRO na unasikika wakati maandishi yaonyeshayo mustakabali wa kazi nzima yakipita kwenye screen. Wimbo huu ni wimbo wa kuabudu unaoelezea ukuu wa Mungu kwetu na kuonyesha unyeyekevu kwa Mungu wetu.

Cameraman: Daniel Kisuu
Studio: Gospel Media Studio
In-house Lighting: Allan Vayle.
Distributed by MBC Hot media
Audio Technician:Gilbert Nkila, Elirehema D. Kissuu, Musa Simon
Executive Director: Elirehema D. Kissuu
Production Manager: Joyce Nkila
Make Up: Joyce Nkila
Produced: 2008

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...