Tuesday, May 1, 2012

Mchungaji ambaye ni shoga awania nafasi inayoachwa wazi na Askofu shogaAskofu V. Gene Robinson
Mch Rev William W. Rich anayeongoza kanisa la Trinity Church lililo chini ya kanisa la Anglikan nchini Uingereza amekuwa mmoja kati ya wachungaji watatu wanaowania nafasi ya uaskofu wa kanisa la Anglikan huko New Hampshire nchini Uingereza. Rev William Rich ambaye anaishi katika ndoa ya kishoga, ana digrii ya mambo ya saikolojia na dini na pia ni mhadhiri katika chuo cha Union Theological Serminary jijini New york nchini Uingereza.

Kwa sasa kiti cha Uaskofu wa jimbo hilo kimekaliwa na Askofu V. Gene Robinson ambaye pia ni shoga, ikumbukwe kuwa miaka nane iliyopita wakati askofu Robinson akisimikwa uaskofu, kanisa la Anglikan lilipitia mijadala mizito kuhusu uhalali wa askofu shoga kuliongoza kanisa la Mungu. Ukichunguza kwa makini utagundua kama mchungaji shoga anapata ujasiri wa kusimama na kuwania nafasi ya uaskofu, ina maana kuna wachungaji wengi ambao ni mashoga katika jamii  hiyo.

Mch Rev William W. Rich
 Askofu Robinson ameishi katika ndoa ya kishoga kwa takribani miaka ishirini mpaka mwaka 2010 pale ambapo patner wake Mark Andrew alipofariki.Biblia pamoja misingi ya kanisa la Kianglikani hairuhusu ndoa ya jinsia moja, lakini kinachowashangaza watu duniani ni kitendo cha kuhalalisha hatua hiyo kwa presha ya utandawazi.

Barani Afrika nchi ya Afrika ya kusini ilikuwa ni nchi ya kwanza kuruhusu ndoa ya jinsia moja, kuna kipindi bunge la nchi ya Uganda liliwahi ijadili hoja hiyo na ilipingwa vikali japokuwa mwaka jana pia hoja hiyo ya uhalali wa ndoa ya jinsia moja ilirudi bungeni humo na haikupita.Katika hili kuna mengi ya kujifunza na kumsihi Kristo aingilie kati kuliko kutumia akili na kufikiri kuwa hapa nchini Tanzania jambo hili haliwezekani.Waliotutangulia waliandika tenzi, Nionapo AMANI kama shwari, ama nionapo shida....., 

Usalama wetu uko katika Kristo Yesu pekee.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...