Monday, May 21, 2012

Yaliyomo kwenye Magazeti ya Kikristo kwa Ufupi


Magazeti ya Tarehe 20.05.2012

 Gazeti laWachungaji wamkalia Kooni Obama
Wachungaji wa Makanisa mbalimbali duniani wamepaza sauti na kumpinga Rais Barak Obama katika mpango unaoelezwa kama kuiangamiza dunia kimaadili na kuitenga na Mungu.Imeelezwa kwamba Rais Obama mara baada ya kutoa tamko la kuhalalisha ndoa za mashoga, alikutana na wachungaji kutoka mabara mbalimbali wakiwemo kutoka Afrika na kuwabembeleza kwa masaa mawili akitumia vifungu vya Biblia lakini walimgomea.
 
Miongoni mwa makanisa yaliyomgomea ni pamoja na ASSEMBLIES OF GOD(AG) lililoitisha mkutano na waandishi wa habari jumanne iliyopita  na kutangaza msimamo mkali wa kuwa HALIKUBALIANI na Obama kwa kuwa mpango wake unakinzana na maandiko matakatifu ya Biblia.


Jaji aagiza Amri Kumi za Mungu Zipunguzwe

Jaji Michael Urbanski wa Marekani amesema kilichosalia ni muafaka utakaopelekea Amri kumi za Mungu kupunguzwa kutoka kumi hadi sita na lengo kuu ni kuondoa nne za kwanza ambazo ni kikwazo katika umoja wa ushirikiano kidini bila kuumizana kihisia.Jaji Michael alifikia hatua hiyo baada ya pande mbili zinazopingana kushindwa kufikia muafaka katika shauri lililofunguliwa mahakamani na shule moja ya wasichana waliokuwa wakipinga uamuzi wa bodi ya shule  wa kufuta Amri kumi za Mungu zilizobandikwa katika shule ya Narrows High School.

Shauri hilo ni matokeo ya hatua ya hivi karibuni ya Marekani ya kupitisha sheria inayokataza Amri kumi za Mungu katika ofisi zote za umma, mahakamani na hata mashuleni isipokuwa kwa kibali maalumu katika mazingira maalumu.

 
Nyakati
Gazeti huru la Kikristo la Kila wiki

Nabii wa Lowasa Afanyiwa Vurugu

Mch Blasius Mabumba wa kanisa la Faith Ministry lililoko Kinondoni Hananasif jijini Dar es salaam hivi karibuni alinusurika kupigwa na aliyekuwa mchungaji wa Kanisa hilo mjini Tanga  Mch Jeremiah Mlaki  katika tukio lililopelekea kuvunjika kwa Ibada baada ya waumini kuamua kuondoka.Mch Mabumba mwaka jana 2011 alitoa unabii kupitia gazeti la Nyakati kwa kusema Mhe Edward Lowasa ndiye atakuwa rais wa Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.

Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowasa

Katika Vurugu hizo zilizotokea mjini katika kanisa hilo mjini Tanga, Mch Mambumba akiwa ameshikilia kipaza sauti aliwaeleza waumini wa kanisa hilo kuwa alikuwa amefika kanisani hapo kwa lengo la kuwataarifu kuwa kuna mabadiliko yanafanywa ambapo mchungaji wa kanisa hilo jijini Tanga Mch Mlaki ataenda kusomea uchungaji na nafasi yake itachukuliwa na Mchungaji ambaye Mch Mabumba likuwa maeongozana naye kutoka Dar es Salaam ambaye alimtambulisha kuwa ni Mch Prosper.

Hapo ndipo vurugu zilianza kwa Mch Mlaki kuanza kufoka kwa ukali kwa kusema baadhi ya maneno ambayo siwezi yaandika hapa.Hata hivyo uongozi wa Faith Ministry unamtuhumu Mch huyo kwa mahubiri ya kuzishambulia dini nyingine kupitia mahubiri yake ambayo amekuwa akiyarusha katika kituo cha Television cha Tanga TV.Kanisa hilo limepeleka barua rasmi kwa mkuu wa wilaya ya Tanga likisema kuwa limemvua uchungaji wa kanisa hilo Mch Mlaki.

Mch Adaiwa kupigwa kwa kumuita Mzee wa Upako Freemasons

Mhubiri mmoja kutoka nchini Kenya James Mbugua  ambaye amekuwa akihubiri sehemu mbalimbali na kufanya kile kinachodaiwa kuwa ni kufichua siri za kundi la Freemasons, anadaiwa kujikuta katika msukosuko mkali maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada kile kinachoelezwa kumhusisha Mch Anthony Lusekelo ambaye wengi humuita Mzee wa Upako na kundi la Freemasons.

Mkenya huyo alijikuta akianza kupigwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Mch Lusekelo jambo lililomfanya akimbie bila viatu.Akiongea na gazeti la Nyakati mtumishi huyo alikana kupigwa ila alikiri kuwa kuna kundi la watu lililotaka kumletea vurugu mitaa ya Kariakoo.Gazeti la Nyakati liliongea na Mch Lusekelo na kumuuliza juu ya hilo la waumini wake naye alisema “huenda ni kweli kwa kuwa watu mbalimbali hufika kanisani kwake kwa lengo la kuombewa na wengine hata hawajaokoka”.


1 comment:

  1. Inawezekana kabisa mtu kupendekezwa uraisi na watu na pia inawezekana kabisa kupingwa. Yote yanawezekana. Mimi ninapokumbuka kesi ya tuhuma za Richmond ambayo ilisababisha baadhi ya watu kujiuzulu, na hukumu ya mahakama iliyoamuru Dowans ilipwe mabilioni yale, na halafu watuhumiwa wanakuwa na ujasiri wa kutaka uraisi kabla ya kujieleza, wengine inatupa shida sana kuamini kwamba yale malipo ya Dowans hayaendi mifukoni mwao.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...