Saturday, May 5, 2012

AFLEWO yafanyika kwa Kishindo,Sasa kufanyika tena Zanzibar


John Lisu aki-lead Kati kati ya wafale


Kati kati ya wafalme Mimi sijaona Mungu kama wewe
Mungu Kama wewe
Bwanaaa, Bwanaaa x 2

Ninavyoandika hii habari nahisi maelfu ya watu wakiniback-up kwenye hiyo chorous hapo juu,hiyo ni nyimbo iliyoimbwa zaidi ya dakika kumi na tano watu wakiwa wima wengine wakinena kwa lugha, na kuna wengine walikuwa mbele wakicheza kwa mfumo wa Kwaito japokuwa mistari ilishindikana kutokana na mlundikano wa watu, huku John Lisu akiongoza wimbo huo na jopo la waimbaji zaidi ya 50 katika AFLEWO 2012. Ni ijumaa iliyopita katika kanisa la City Christian Centre lililoko upanga amkako kwa mara ya pili usiku wa  Africa Lets Worship(AFLEWO) ulifanyika. Kwa kila mtu aliyehudhuria Tamasha hilo atakubaliana na Hosanna Inc kuwa lilikuwa ni Tamasha la pekee toka mwaka huu uanze wa 2012.

Akiongea katika mkesha huo mmoja wa walezi wa Aflewo nchini Pastor Paul Safari alisema “Muda umefika kwa AFLEWO kufanyika zanzibar,na hii imekuja juzi wakati tuko redioni kuna mtu alipiga simu kutoka zanzibar alikuwa akilia kwa kusema nyie kila siku mnafanyia matamasha Dar es salaam tu kila siku Dar vipi na huku!!, ki ukweli jinsi alivyokuwa akilia kwenye simu uchungu ulInipata ghafla na kumwambia ZANZIBAR TUNAKUJA.

Pastor Safari aliendelea kusema sasa naomba uniunge mkono wewe uliyefika leo, AFLEWO tunaenda Zanzibar, ukisikia tunaenda Zanzibar andaa nauli yako tutafika na kufanyia tamasha nje usiku mzima tukimsifu na kumtukuza Mungu pasipo kulumbana na mtu kesho yake asubuhi tunarudi Dar es salaam,naomba msinicheke kwa miaka zaidi ya ishirini niliyoishi hapa Dar es salaam sijawahi fika Zanzibar”

Wakati akifungua mkesha huo askofu mkuu mstaafu wa TAG Askofu Mwanisongole alisema ni furaha namna gani kuona watu kutoka madhehebu mbali mbali wakifanya kama mbinguni, wakikaa pamoja na kumtukuza Mungu.Askofu Mwanisongole aliendelea kusema kwa sasa ni vigumu sana leo kuwakuta maaskofu kumi wakikaa pamoja na kuzungumza, lakini kutanyiko la Aflewo linaonyesha wazi kuwa hata maaskofu wanaweza kukaa pamoja kwa kuwa washirika wao wanakaa pamoja na kuabudu.

Baadhi ya wadada waliounda AFLEWO Praise team 2012 wakiingia jukwaani

Ibada Ikiendelea
 
Praise leader na muic director wa AFLEWO 2012 Bro Sam akiwa on stage

Bishop Mwanisongole kushoto  akifungua mkesha  kulia ni John Kagaruki
Pastor Safari akiongea katika Mkesha huo
Musician The Great Sam Yona with lead Guitar na Anointed Bale kwenye KeyboardUtukufu kwa Mungu


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...