Monday, May 14, 2012

Pendekeza Jina la Mwanamuziki wa Tanzania kwenye Tuzo za Muziki wa injili Barani AfrikaTanzania Christian Bloggers Network

Presents


Amka Campaign

Amka Campaign, ni Kampeni maalumu ya kuwashawishi watanzania wawapigie kura wanamuziki wa injili nchini ili kuibuka washimdi katika TUZO ZA MUZIKI WA INJILI BARANI AFRIKA.(AGMA). Lengo hasa la Amka Campaing ni kuzidi kuutangaza Muziki wa Injili kutoka Tanzania kwa bara zima la Afrika na Dunia kwa ujumla.


Kwa muda sasa watanzania wamekuwa hawajui lolote kuhusu namna ya kushiriki katika tuzo hizo ingawa wanapenda. Toka tuzo za Muziki wa injili Barani Afrika zilipoanza mwamko kwa watanzania kushiriki umekuwa mdogo, na hii ni kutokana na sintofahamu kwa wadau wa muziki huo kuanzia kwa

1.Wanamuziki wenyewe
2.Mameneja wa wanamuziki hao
3.Waandishi wa habari na Kanisa kwa ujumla.

Hivyo basi Kuanzia tarehe 21st April 2012 mpaka 21May 201 ni muda wa kupendekeza washiriki na tumebakiwa na takribani wiki moja tu ya kupendekeza, ili kupendekeza unatakiwa

a)Uandike kategori ambayo unataka mwanamuziki wa injili kutoka Tanzania aingie
b)Jina la mwanamuziki mwenyewe kisha utume jina hilo na
c)kazi yake aliyofanya kwa mwaka 2011 April -2012April  na
d)sababu ya kumchagua kwenda  
nominations@africagospelawards.com

Mfano
Category: BEST ARTISTE OF THE YEAR EAST AFRICA
I do nominate : Christina shusho from Tanzania
Song:Thamani ya wokovu wangu
Reason:Her songs has restores many souls to the Kingdom of GOD

Kisha unatuma kupitia email tajwa hapo juu
Vipengele(categories) ambavyo unatakiwa kuchagua mtanzania wa kutuwakilisha ni pamoja na

1.      GROUP/CHOIR OF THE YEAR
2.      MALE ARTISTE OF THE YEAR
3.      FEMALE ARTISTE OF THE YEAR
4.      BEST ARTISTE OF THE YEAR EAST AFRICA
5.      EVENT OF THE YEAR


Kwa kufanya hivyo utakuwa umemuwezesha mwanamuziki wa injili kutoka nchini kuingia kwenye Nomination pull ya Tuzo hizo.Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 7th July 2012 jijini London nchini Uingereza, wakati zoezi la kupiga kura baada ya nomination list kutoka litaanza tarehe 1May-30june 2012.
.

Umoja wa mabloggers wa kikristo nchini unaamini kuwa, watanzania kwa pamoja kwa namna moja au nyingine tunaweza kuutangaza muziki wa Injili kutoka Tanzania.Ili kuweza kupata undani wa tuzo hizo unaweza tembelea 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...