Sunday, May 13, 2012

Yaliyomo kwenye Magazeti ya Kikristo jumapili hii


Magazeti ya Kikristo Jumapili hii 13.05.2012

Gazeti la


- Anguko la kina Ngeleja, Kakobe Avunja Ukimya
Hatimaye Askofu mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible fellowship Askofu Zakaria Kakobe, ambaye amekuwa kwenye maombi mazito kwa zaidi ya Miaka miwili akijifungia chumbani akifanya maombi huku akivunja Ibada zote za kawaida kanisani kwake na kubakiza ibada za jumapili, amevunja ukimya na kuonya kuwa yaliowapata mawaziri akiwemo aliyekuwa waziri wa Nishati na madini William Ngereja pamoja na katibu wake David Jairo ni rasha rasha tu kwani Kimbunga bado kinakuja.

Chanzo cha habari cha gazeti la Jibu la Maisha kutoka kanisani hapo kinasema Kakobe amevunja ukimya kwa kuwaambia watu walioko karibu naye kuwa yaliyowapata mawaziri hao ni mvua za rasha rasha kwani Kimbunga Kamili kinakuja kwa kuwa Mungu Yu Hai na huwasikiliza wanaomlilia.Hivi karibuni Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko kwa kuwaengua baadhi ya mawaziri akiwemo Mhe Ngereja huku David Jairo alikuwa tayari keshaondoshwa katika nafasi yake ya ukatibu wa wizara hiyo.

Askofu huyo amebaki katika maombi yasiyo na kikomo mpaka pale kimbunga hicho kitakapowakuta wale wote wanaoamini kuwa walishiriki kulazimisha umeme mkubwa kupitishwa kanisani hapo na kuvuruga mipango ya kanisa hilo ya kujenga Kituo cha Television kwa ajili ya kuhubiri injiri.Imeelezwa kuwa hasira ya askofu Kakobe imekuja baada ya kutaka kuokoa Millioni 500 walizokuwa wakitumia kwa matangazo ya Television kutoka vituo mbalimbali vya Television.

`Kwa Kuliona hilo Askofu Kakobe alichangisha kiasi cha mIllioni 800 ili kujenga kituo chake cha Television zoezi ambalo lilivurugwa na hatua ya serikali kupitish umeme mkubwa karibu na Kanisa hilo jambo ambalo kiutaalamu linaathiri urushwaji wa matangazo wa Kituo cha Television cha Kanisa hilo endapo ungeanza.
Aidha Askofu huyo aliwahi kumwandikia Waziri Ngereja ujumbe wa kumwomba waziri Ngereja kusitisha zoezi la kupitisha umeme huo karibu na kanisa hilo, ujumbe hiyo ulisomeka kama ifuatavyo

Mh Ngereja, katika barabara ya kutoka Iringa kwenda Mbeya baada ya njia panda ya kwenda Tosamaganga kabla ya kijiji cha Tanangozi, kuna Kijiji cha Isimila hapo kuna makaburi mawili yaliyopo pembeni mwa barabara upande wa kulia kama unaenda Mbeya. Makaburi haya ni ya Machifu wa Kihehe, Tanesco na Serikali waliheshimu makaburi hayo kabla tu ya makaburi hayo walichepusha umeme wa KV 11, na kuvusha nguzo upande wa pili wa bara bara.

Baada ya kuvuka walipeleka umeme mpaka mbele ya makaburi na kuvuka tena mpaka upande wa pili kuendelea na safari.Laini ya umeme imepita pale kwa mfano wa harufi  “U”.Sababu inayoeleweka kwa watu ni kutokana na sababu za Uchawi hivyo walishindwa kuuvusha umeme Makaburini. 

Serikali isiyoamini uchawi ikachepusha line ya umeme upande wa pili wa barabara.Bila shaka serikali yetu itaheshimu zaidi makanisa kuliko makaburi.Kwa jinsi hii line ya umeme inaweza kuchepuka mkabala na kanisa letu kisha ikarudi tena upande huo baada ya kuvuka.

Hii inaweza kufanyika hata bila kupitia underground kwa ajili ya cost Reduction, hili likifanyika litanipa furaha na faraja tele kwa sababu upande wa pili una zaidi ya mita 30, hivyo haliwezi kuwa tatizo kwa mitambo ya TV, na hoja zetu zote zitakuwa Cancelled na hivyo kutakuwa hakuna tena mgogoro.

- Cameroon alibip, Obama amesujudia sanamu
Mwaka jana waziri mkuu wa Uingereza Mhe David Cameroon alitumwa kulibip bara la Afrika na masalia ya wastaarabu sehemu mbalimbali duniani, akatimiza wajibu wake kwa kusema kuwa mataifa yanayopinga ushoga yataadhibiwa kwa kunyimwa misaada kutoka kwa taifa hilo kubwa.Sauti za watu zinazopinga ushenzi zikarindima kumlaani sana.Uganda ikajaribu kutangaza sheria ya Kunyonga mashoga lakini haikuchukua muda ikalainishwa na kufutilia mbali muswada huo.

Rais Barak Obama Kulia akiwa kwenye mahojiano na Television ya ABC

Wiki jana Rais Obama wa Marekani alisema kupitia ABC Television kuwa “ Haya ni mawazo yangu, nimefikiri sana na kushauriana na watu wengi.Nimehudhuria mijadala mingi na mawazo yangu yamekuwa yakibadili msimamo wangu, sasa naamini wakati umefika kwa wenzetu hawa wenye ndoa za jinsia moja kuanza kutambuliwa na kupewa haki zao sawasawa na wanandoa wengine. Hapo awali Rais huyo alikua akipinga vitendo vya kishoga, alichokifanya Obama sasa ni kumwacha Mungu na kuamua kuisujudia sanamu kama ile aliyokataa kuisujudia Daniel mbele ya mfalme Nebukadreza

- Kundi la Shetani la ILLUMINATI lawinda Vijana wa Tanzania 
Shindano la Kuvaa na kuimba kama mwanamuziki mashuhuri wa kike wa Marekani RIHANA,limehitimishwa kwa mbwembwe za aina yake jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Dar Live.Kwa msichana aliyelelewa katika maadili mazuri anaweza kubaini RIHANA hawezi kuwa msichana wa Kuigwa kwa namna ya Kuvaa, Kucheza na kuimba.Rihana, Kanye West, Jay Z, Madona si wanamuziki wa kuigwa, Rihana  ni mwimbaji aliyetoa kafara maisha yake ili kumwabudu shetani pasipo kificho.

Naweza sema Rihana huyu ni mtumishi mtiifu na mwaminifu wa mkuu wa giza “Ibilisi” huku akitumia kikamilifu muziki kuwaandaa watu kuipokea serikali moja ya dunia ambayo mhimili wake mkuu ni ibada za Kilusiferi.Kwa kuwa mashindano hayo yalikuwa yakimhusu muhusika mmoja yaani Rihana,kwa hakika mabinti hawa walikuwa wakishindana namna ya kuvaa uhusika wa shetani.Hili lilikuwa shindano la Kuvaa, Kuimba,kucheza kwa staili yya shetani.

 Nyakati
Gazeti huru la kikristo la kila wiki

- T.B Joshua Aitikisa Tanzania
Kiongozi wa Kanisa la Synagogue Church of all Nationals(SCOAN) Nabii Temitope B Joshua amedhihirisha kuwa na wafuasi wengi hapa nchini ambapo siku chache baada ya gazeti la Nyakati juu ya ukosoaji uliotolewa na watu mbalimbali dhidi ya unabii alioutoa kuhusiana na kifo cha Rais wa Malawi marehemu Bingu wa Mutharika.Wakosoaji wa unabii huo walisema unabii huo una mkono wa mashushushu wa nchi za Magharibi waliotumia ili kutekeleza mauaji ya Rais huyo.Wengine wakisema si wa kiroho maana kwenye biblia hakuna nabii aliyetoa unabii wa kifo tena mbele za watu.

Baada ya kutoka habari hiyo, mamia ya wafuasi wake kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wamejitokeza na kupinga ukosoaji huo kitendo kinachoashiria kuwa mtumishi huyo wa Mungu  ana kundi kubwa la watu nchini linalokubaliana na huduma yake.

- Askofu Kumvaa Rais Jakaya Kikwete
Askofu kuu wa kanisa jipya la Kianglikana la injili Tanzania(KAKT) Ainea kusenha ameazimia kwenda kumuona Rais Jakaya Mrisho Kikwete ili afuatilie usajili wa kanisa lake ambao anadai umekwamishwa na watu wenye dhamana ya suala hilo kwa muda wa miaka mitatu.

Kusenha aliondolewa kutoka katika kanisa la Anglikana nchini kwa tuhuma mbalimbali na baadaye kulituhumu kanisa hilo hususani Dayosisi ya Cenral Tanganyika kuwa linaunga mkono ushoga.Kusenha aliwashawishi baadhi ya waumini wa kanisa la Anglikana nchini kuanzisha kanisa la KAKT.Hata hivyo japokuwa kanisa hilo linaendesha shughuli zake bado halijasajiliwa na serikali.

Mch kusenha alisema mpaka sasa kanisa hilo lina maelfu ya wafuasi katika ukanda huu wa Afrika mashariki pamoja na kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo hivyo haoni sababu ya kanisa hilo kukosa usajili.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete

- Nabii: Wanaotaka Urais 2015 Njooni
Mtumishi wa Mungu Mchungaji Alphonce Temba wa huduma ya Panuel ya jijini Dar es salaam amabye amekuwa akiwatabiria viongozi mbalimbali juu ya uwezekano wa wao kuwa viongozi wa nchi, amesema bara la Afrika linasua sua kimaendeleo kutokana na viongozi wake kuwekwa madarakani na waganga wa kienyeji jambo ambalo ni chukizo kwa Mungu.

Katika kuondokana na dhana hiyo mchungaji huyo ambaye pia ana karama ya kinabii, amesema yuko tayari kufanya maombi na mtu yeyote anayetaka kuwa Rais nchini Tanzania na barani Afrika ili kuondokana na viongozi wasiotokana na Mungu.Alisema lengo la kutaka kuona marais wa Afrika wanatokana na Mungu ni kumyima shetani sifa ambazo mara nyingi amekuwa akizipata.


Msema Kweli
Gazeti la Kikristo la Kila Wiki

- Mapdri waliooa waendelea kutumika kanisa Katoliki
Kwa kile kinachoelezwa kuwa ni uhaba wa Mapadri katika kanisa katoliki unaotokana na wimbi wa mapadri hao kuamua kuondokana na maisha ya useja na kuamua kuoa.Kanisa hilo limebuni mbinu mpya ya kuendelea kuwatumia mapadri hao katika shughuli mbalimbali za Kiroho,japokuwa  kanisa hilo limekuwa likikanusha kukumbana na uhaba wa mapadri.

Gazeti la Kanisa katoriki la CATHOLIC HELARD la jijini Vatcan yaliko makao makuu ya kanisa hilo limesema kuwa, makao makuu hayo yametoa maelekezo kwa kwa Dayosisi zake ulimwenguni kuhakikisha kuwa mapadri walioamua kuoa wanaendelea na utumishi maalumu kanisani ambao umewekewa mipaka.Kwa mantiki hiyo mapadri waliooa hawataruhusiwa kuongoza Toba na Ibada lakini wataruhusiwa kutumikia parokia kama waalimu, ikiwemo pia kuwasaidia mapadri wakati wa ibada ya sakrament ya meza ya Bwana  jarida la CATHOLIC HELARD limeeleza.

- Maombi ya Kanisa yaibua wachawi Mbeya
Zaidi ya watu kumi wanaosadikiwa kuwa ni wachawi akiwemo baba moja kuzikwa kwenye kaburi huku akiwa mzima baada ya kumuua mdogo wake na mwingine kukutwa kwenye barabara ya Mbalizi huku akiwa mtupu baada ya kuishiwa nguvu za uchawi.Hii ni  kutokana na maombi yanayoendelea kufanyika kutoka katika kanisa la Mlima Sayuni lililopo Uyole jijini humo linaloongozwa na Nabii Adamson Mwaisumo kutoka Nairobi nchini Kenya.

Mwaisumo amesema ametumwa na Mungu kuteketeza wachawi kwa njia ya Maombi ambao kazi yao ni kuharibu maisha ya watu.Aidha amesema kumekuwa na baadhi ya waganga wakimuomba msamaha kwa kukiri kuwa watauacha uganga huo akiwemo mganga mkuu wa maeneo ya Makunguru jijini humo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...