Thursday, May 17, 2012

Tatoo ya Lill Wyne yenye Namba 666 yazua utata


Lil Wyne
 Lil Wyne ni mwanamuziki wa hiphop kutoka nchini Marekani na anafanya muziki wa duniani kwa muda mrefu sasa, umahiri wake katika kughani pamoja na Life stayle yake yenye vituko vingi na ghasia za kukimbizana na Polisi ni baadhi ya vitu vinavyomfanya Mwanamuziki huyo kujulikana sana duniani.kumekuwepo na utata mkubwa juu ya tatoo aliyoiweka Lil wyne  juu ya sikio lake la kushoto ingawa wengine manasema ni kutokana la mwanamuziki huyo kupenda siasa za Bwn Herman Cain na akaweka tatoo hiyo kama ishara ya kumsapot kitu ambacho si rahisi kuingia akilini kwa wengi.

Ni wazi kwamba wafuasi wa kundi la Freemasons hutumia namba katika mambo yao mengi, na namna wazitumiavyo, huikanganya jamii isiyokuwa na ufahamu juu ya utumiaji wa namba(tarakimu) katika shughuli na mipango ya kundi hilo kila uchao. Ukiiangalia tatoo aliyoiweka mwanamuziki huyo inasomeka kama 999, ila wajuvi wa mtandao huo bado wanaamini kuwa amepindisha na ni 666.Sababu kubwa ya Lil wyne kufanya hivyo bado haijajulikana na hili ni fumbo kwa yeyote aliyepata kuiona tatoo hiyo.

Tatoo yenye utata


1 comment:

  1. I HATE FREEMASONS BEYOND EXPLANATIONS, I REAL HATE THEM I EVEN WISH THEM DEATH!

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...