Friday, May 11, 2012

Uche agu asema Yuko Mbioni Kufunga Ndoa


Uche-agu maarufu kama Uche wa Double Double

Mwanamuziki wa injili raia wa Nigeria aishie na kufanya huduma nchini Afrika ya Kusini Uche-agu maarufu kama Uche Double Double kutoka kundi la Joyous Celebration, amesema kwa sasa yuko mbioni kufunga ndoa, akiongea na kituo kimoja cha Television jijini Amsterdam Uche amesema kwa sasa yuko mbioni kufunga ndoa japo ni mapema kuliongelea hilo.Akaendelea kusema “Ndoa ni sio kitu cha kukimbilia,kama ukiamua kuikimbilia pasipo kujipanga utawahi pia kuikimbia  baada ya kuingia ndani yake, lazima uhakikishe kuwa umefanya uamuzi  sahihi.”

Uche ambaye wiki mbili zilizopita alikuwa jijini Nairobi akiambatana na KEKELETSO PHOFOOLO maarufu kama Keke kihuduma, aliwaasa wanamuziki wa injili kokote Duniani na kusema maisha yao binafsi lazima kwanza yawe connected na Mungu na pia yaendane na Kile wanachokiimba, kama muimbaji huwezi sema fuata ninacho kiimba lakini usifuate ninacho kifanya

Uche akaendelea kusema mimi ni mburudihsaji pale ninapoimba na kucheza watu wanafurahi, lakini jiulize baada ya hayo yote nini kinatokea?, je ugonjwa wako bado upo?Je kuna kitu kimetokea ndani ya moyo wako?, Je moyo wako umepeleka tukuzo kwa Mungu? Nimekuwa nikijiuliza maswali haya na kimsingi hii ndiyo tofauti kubwa kati ya muziki wa duniani na muziki wa injili.Wanaoimba muziki wa duniani wao hutafuta pesa na kuishi maisha mazuri wakati muziki wa injili huwaleta watu karibu na Mungu.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...