Sunday, May 27, 2012

Kanisa la TAG na Gari la Mchungaji Vyachomwa moto ZanzibarUsiku wa kuamkia leo mjini Unguja mtaa wa Kariakoo kumefanyika tukio la kusikitisha ambapo watu wasiojulikana wamelichoma moto Kanisa la TAG lililopo mtaani hapo pamoja na gari la mchungaji wa kanisa hilo Mchungaji Dickson Maganga.Jambo hili limetokea siku ya leo tarehe 27.05.2012 ambayo ni siku maalumu ya maombi kwa dunia nzima huku dhima ya mwaka huu ni kuombea ukristo katika nchi za Kiislamu.

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) liliopo mtaa wa Kariakoo mjini Unguja limechomwa moto jana usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana

Gari la Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop Dickoson Maganga lililochomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa jana katika eneo la Kariakoo nje ya kanisa hilo ambapo uharibifu wote unaelezwa kuwa umegharimu shilingi millioni 120. Picha/ZanzibarYetu
1 comment:

  1. Kwa asili vita ya waislam ni ya mwilini sana lakini kwa maombi tutawaleta wengi kwa Yesu. tuwasamehe maana hawajui walitendalo

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...