Wednesday, May 23, 2012

Don Moen Kusherehekea kufikisha “LIKES” Milion Moja kwenye Facebok kwa kugawa album yake bure


Doen Moen
Mwamamuziki mkongwe wa nyimbo za Injili duniani Doen Moen kuanzia tarehe 5 june atakuwa akisherehekea pamoja na fans wake kwa kufikisha jumla ya Likes 1Million katika page yake ya Facebook.kwa mujibu wa Doen Moen mwenyewe amesema siku hiyo atakuwa akichart LIVE na marafiki zake wa Facebook kwa muda wa masaa arobaini na nane(48).Katika charting hiyo mtumishi huyo atakuwa akiongelea kazi zake na huduma na pia tatoa nafasi ya watu kuuliza maswali.

Sambamba na hilo Doen Moen atakuwa akigawa album yake bure aliyoiita “Hymnbook Giveaway” ambayo ndani yake amerekodi album yake mpya yenye nyimbo za tenzi ambazo zimekuwa zikiubariki sana moyo wake kwa miaka mingi hivyo atakuwa akishare na mashabiki wake.Mpaka sasa haijulikani ataweza vipi kuchart  na idadi kubwa ya watu ila Hosanna Inc inaamini kwa kuwa Don amelikweka hili mbele ya watu pia atakuwa na njia ya kukabiliana nalo kitaalamu.Kwa wale wote wanaotaka kuipata album hii ya Hymnbook  Giveaway Bure wanaweza 
kujiandikisha kwa kugonga hapa


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...