Sunday, May 20, 2012

Baada ya Mch Faustine Munishi kutoa unabii kwamba Mh Raila Odinga atakuwa Rais wa nne wa kenya,Shirika la taifa la ulinzi nchini Kenya lamuonya mchungaji huyo.


Mch Faustine Munishi
Mchungaji Faustine Munishi mwenye asili ya Tanzania aliyechukua uraia wa Kenya hivi karibuni alitoa unabii kama alivyouita yeye na kusema wazi kuwa makamu wa Rais wa nchi ya Kenya Mh Raila Odinga ndiye atakuwa Rais wa nne wa Kenya baada ya rais wa sasa Mh Mwai Kibaki kumaliza muda wake.Baada ya kutoa unabii huo shirika la ulinzi la nchi hiyo Kenyan National Security Inteligence Service (NSIS) limemuonya Mchungaji huyo juu ya mtazamo wake wa kisiasa.

Mchungaji Munishi kwa muda mrefu sasa amekuwa akiandika post(status) zenye mlengo wa kisiasa kwenye page yake ya facebook pamoja na mtandao maarufu nchini wa jamii forum.Baada ya kutoa unabii juu ya Raila Odinga, Mchungaji Munishi aliamua kuuweka wazi kwenye facebook hasa baada ya shirika hilo la ulinzi kumzonga na kumtaka afunge akaunti yake faceook.Kama vile haitoshi Mch Munishi alipost hii status kwenye page yake na inasomeka kama ifuatavyo.
“INTELIGENCY YA KENYA NSIS WANIONYA NITOKE FaceBook AU WANINYAMAZISHE”. 

Kilichowafanya NSIS watume mtu kumuonya Mchungaji anyamaze au anyamazishwe, ni Pale aliposema Kenya itapona wakati historia itakapojirudia. Uhuru Kenyata aseme Raila Tosha kama vile mzee Jaramogi alivyosema Jomo Kenyatta Tosha. Na mtoto wa Jaramogi akasema KIBAKI TOSHA. Sasa ni zamu ya Kenyata na KIBAKI waseme RAILA TOSHA. Hayo ni maoni unabii na maono ya Mchungaji Munishi. Sinyamazi Na MUNGU aliyenipa unabii huu atanilinda wasininyamazishe. Amen.

Source: Nairobee.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...