Saturday, May 26, 2012

Mitazamo ya watu mbalimbali baada ya Gazeti la AN NUUR Kuandika “HATUNA IMANI NA BARAZA LA MITIHANI”Gazeti la AN NUUR Saut ya Waislamu ni gazeti la Kiislamu na toleo yake la Jana 25.05.2012 lina kichwa cha habari kisemacho “HATUNA IMANI NA BARAZA LA MITIHANI” Yameelezwa mengi humo ndani kama hints za picha hapo juu inavyoonyesha lakini ili kubalance story ime-ibidi Hosanna Inc kuwa katikati na kupost maoni ya watu kuhusu hicho kilichoandikwa katika gazeti hilo.

Baada ya kutoka gazeti hilo jana ijumaa, blogger na mwanahabari mkongwe nchini Dr Majid Mjengwa anayemiliki blog ya www.Mjengwa.blogspot.com aliiweka habari hii kwenye blog yake.Mjengwa ambaye pia ni muislamu  alijaribu kuweka wazi mtazamo wake kwa kusema waislamu “tumezidi kulalamika sana” na akaeleza mengi.Baada ya Mjengwa kutoa  mtazamo wake, watu wengi kutoka dini zote waislamu kwa wakristo wametoa mawazo yao juu ya hilo na hapa ninayaweka kama yalivyo.

Mchangiaji wa Kwanza
Allah'u Akbar!haya ndugu Waislamu wa Alnuur mnalo? Yaani pengine ukiongea wewe muislamu msomi wa PhD tena wa chini ya baraza hilohilo wanalolalamikia Waislam wenzio wanawezakukuelewa, ingawa jiandae pia kuitwa Qafir. Pole, ila ukweli watausoma tu hata kimyakimya. Nimesoma chuo chenye mfumo wa kiislamu, nilichokishuhudia huko ni majungu kila baada swala ya Ijumaa kitu ambacho hutakaa ukikute makanisani (msikiti ulikuwa chuoni).,na hao ni wasomi unaodhani labda kwa elimu waliofikia majungu misikitini kuwasengenya wasioamini dini yao wangeachiwa mashehe ubwabwa wa mitaani, ila wapi!!

Siri ya shule za wakristo ni Mungu, Nidhamu na Bidii na Kazi full stop! Majungu ni mwiko, NECTA mnawasingizia tu, hata awekwe imam apaongoze mtalalamika tu. Kukata mzizi wa fitina nashauri ndugu waislam wapeleke kwa wingi watoto wao shule za kikristo waone matokeo.

Na tatizo jingine naona ni la kihistoria, hivyo malalamiko hayawasaidii, leo kila kanisa kwa mfano Katoliki lina shule za awali na japo msingi, na karibu yote yalikuwa na shule za msingi zikataifishwa na serikali( hili ni sawa kabisa), ukizingatia serikali hy ilikuwa chini ya mkristo mwenzao, ila lengo ni elimu kwa wote, hadi vyuo makanisani (vingi vya ufundi mbalimbali), acha mahospitali. Yaani tutaona kanisa limewekeza toka zamani ktk elimu na maendeleo, waislam majungu na kulalamika hata misikiti ni nadra kukuta uliomalizika kujengwa(tafiti)kama ni wa ghorofa unaishia katikati kwa chini juu nusunusu kisa kugombea pesa za ujenzi toka Uarabuni.

Wapatikane waislam 10 kama wewe wakaelimisha wenzao wakaamka tukapumzika na kelele za miaka nenda rudi bila kujibidiisha kufika walipo wenzao

Mchangiaji Mwingine
Watoto wa mama wa kambo kulalamika jadi yao

Mchangiaji Mwingine
kaka umeongea point kali sana, kama waisilamu wamesoma basi nadhani wamesikia, ujinga wa kulalamika kila siku hadi sasa rais muisilamu makamu yakhe sasa mnataka nini jamaniiiiii??? au mnataka maisha kama ya ndugu zenu waaarabu ya kuuana kila siku wakati wote waarabu na ni waisilamu?

Mchangiaji Mwingine
Huna uisilamu wowote na ungekuwa muisilamu usingeandika maneno hayo.Kwani hujui kama waisilamu wanachakachuliwa mitihani tokea enzi hizoooooooooo.Unajifanya muisilamu ili kumdhalilisha muisilamu????Inna lillahi wainna ilaihi raajiun kwani kafa mtu hapa???Huyo mhariri anajua anachokiandika kwahiyo kama unaweza nawewe kafanye kazi ya uhariri.

Mchangiaji Mwingine
Bora mwislamu ndiye katoa mada hii make angekuwa mkristu,hapa kungewaka moto.waambie ndugu labda wataelewa.

Mchangiaji Mwingine
Acha unafiki mada yako jinsi ulivyoiandika ni dhahili lengo lako kuponda waislam na uislam wenyewe, unajiita eti mwislam, may be mwislamu wa birth certificate.ajabu hata hujui nani alieanzisha historia ya kutumia namba kwenye mitihani.finally ww si mwislamu umeamua kujifanya mwislamu mnafiki tu wewe.

Mchangiaji Mwingine
Mi ni muislam kamili.NImekuwa nikijiuliza kwa nini shule kama alharamain,kinondoni Muslim au shule yoyote ya kiislam haipo kwenye 10 bora za kitaifa?hivi mnafahamu ubungo Islamic primary inaishia drs la ngapi? Hivi mshajiuliza sie waislam tuna hospital kubwa ngapi za maana Kama KCMC au bugando maana hata Zanzibar hakuna na kule dini yetu in asilimia 95?mshajiuliza mbona viongozi wetu waislam walioko serikalini au hata wasomi wenzetu wakiislam Kama maprofesa hawawapeleki watoto wao kwenye shule zetu za kiislam? Hata aw Kikwete alimpeleka kifungilo/mazinde hata Kawawa?NAOMBA WAISLAM WENZANGU TUTAFAKARI HAYO MASWALI HAPO JUU NDIPO TULALAMIKE

Majid Mjengwa

Mchangiaji Mwingine
SASA NYIE RAIS MWISLAM, MAKAMU MWISLAMU,WAZIRI WA ELIMU MWISLAM, KATIBU MKUU ELIMU MWISLAMU,NAIBU WAZIRI TAMISEMI ANAESHUGHULIKIA ELIMU MWISLAM.......BADO TU MNAONEWA KWENYE MITIHANI??SASA MTAJIKWAMUA VIPI KAMA HATA HAO MLIOWWAWEKA KOTE HUKO HAWAWASAIDII?????

HIVI USHAJIULIZA KWANINI HATA WAISLAMU HAWAPELEKI WATOTO WAO KWENYE CHUO CHENU CHA KIISLAMU CHA MOROGORO?PAMOJA NA KUPEWA MAJENGO LAKINI HAKUNA KITU MNAFANYA PALE ZAIDI YA MAJUNGU.NDUGU ZANGU ELIMU HAINA UJANJA NI KAMA MPIRA WA MIGUU HUKUSOMA NA KUANDALIWA VEMA USITEGEMEE KUFAULU.HIVI ZILE SHULE ZENU ZA KIISLAMU DAR KWANINI WANASOMA WATOTO WA WAISLAM WALIOHOI,WALE WENYE UWEZO WOTE WATOTO WAO WAKO ST.MARIAM,ST.FRANCIS,MAZINDEJUU,KIFUNGILO NK?AU 

KWANINI SHULE YA FEZA INAFAULISHA VIZURI PAMOJA NA KUWA NI YA WAISLAMU (WAISLAMU WA ULAYA WALIOSTUKA LAKINI SIO WA USHENZINI MIDDLE EAST)?MKIANZISHA SHULE AU CHUO MNAANZA NA UBAGUZI WA DINI WENZENU WAKIANZISHA SHULE ANASOMA YEYOTE BILA KUWEKEWA ULAZIMA WA DINI ILA MAADILI.MTALALAMIKA SANA FANYENI TAFITI MTAJUA KINACHOWAMALIZA,MTAISHIA NAFASI ZA KISIASA WAKATI WENZENU WAMEJAZANA KWENYE NAFASI ZA UTENDAJI NA KULE NDIO MAISHA YANAELEWEKA KWA MUDA MREFU DUNIANI KULIKO KWENYE SIASA AMBAKO NI WACHACHE NA KWAMUDA MFUPI.

SOMENI WAUGWANA WAARABU WAMEKAA ZANZIBAR PALE MIAKA NA MIAKA HAKUNA SHULE INAYOELEWEKA ZAIDI YA VIJIWE MAARUFU VYA KAHAWA NA MAJENGO CHAKAVU.HALAFU HUKU KUANZA KULILIA ELIMU ZA MAKAFILI MUDA SI MREFU MTALILIA NA KITIMOTO NYIE....SIMJIFUNZE ELIMU YENU ILE YA RIVASI?

Mchangiaji Mwingine
Mtoa mada aweza kuwa muislamu jina lakini sio muumini, kwani hata kwenye Quran imeandikwa kuna waislamu na waumini.

Mimi nakuomba badala ya kuanzisha zogo na kashfa kwanini usitumie hiyo elimu yako kuwasaidia kuappeal ili hiyo mitihani yao isahihishwe upya na indipendent board? Maana haiyumkiniki ikawa wakristo tu ndio wana akili na uwezo wa kufaulu na wengine hawana.

Hao bwana kiboko yao wakienda shule nje ya nchi majority wanavyotokota, kuandika kitu kikaeleweka hawawezi, wanaishia kutulipa pesa tuwaandikie kazi zao. Tulizeni ball tutamwaga siri zenu bure humu na tudegree twenu feki twa kubebwa kuanzia papers mpaka dissertation. Ndio maana nchi iko stagnant haiendelei na kujidai na usomi wenu, miaka nenda miaka rudi hamna cha maana mnachofanya wala mlichovumbua.

Na asimame hapa mmoja wenu aseme kagundua japo dawa ya kuzuia watoto kuharisha seuze ya kutibu malaria!! Give us a break acheni matusi na kashfa wakati na nyie vichwani hamna kitu!!

Mchangiaji Mwingine
Asante mtoa mada mimi nilibadirisha dini nikaingia Uislam lakini jamani kilasiku kulalamika kama watoto wadogo hawana hoja na ndio maana mimi sisomagi hili gazeti hata wanangu nimewambia wasiyafate hayo mambo yasiyokuwa ya msingi kazi kulalamika tu bila sababu asante mwislamu mwenzangu

Hosanna Inc inaamini tunaweza tofautiana dini, mitazamo juu ya mambo mengi yanayoendelea katika nchi yetu tulivu.Cha msingi ni kudumisha AMANI YETU na kuheshimu misimamo ya makundi na dini mbalimbali tulizonazo hapa nchini.

2 comments:

 1. waislam acheni kubishana nao kama wamekuwa madarakani muda wote wakiiba raslimali za nchi na kujinufaisha. lakini leo hii wanabisha hayo wambie si tuna chuo kimoja tu wao wana 26 sasa wao ndio industry ya mafisadi na watu wasio kuwa wazalendo na nchi kwasababu wanapitishwa tu kwenye hiyo mitihan si wajuzi(vyuoo vikuu vya kikirsto ni mitambo yakuzalisha mafisad wanyonyaji kama walivyo kuwa wakoloni nchini na ndo mana mifumo mingine inayo jali haki wanaipinga nakukwamisha waislam kokote dunian hasa mmarekani nawafuasi wake kila siku haishi kuchokonoa nchi za kiislamu mbona haendi vatican kuliko na udiktete au udikiteta nikwa waislamu tu.wanaiba kila siku mabilion ya fedha kujinufaifa kwahili mfumo huu ni mbaya sana wanahila nyingi sana kuupiga uislam so tuamke tufanye haki watasaliti amri

  ReplyDelete
 2. INAWEZEKANA MWAKO WA KUSOMA BADO NI MDOGO MIONGONI MWA WAISLAM LAKINI NECTA KUNA TATIZO KUBWA TU.
  KILA MWAKA KUNA UVUJAJI WA MITIHANI
  NA KWA USHAHIDI WA WANAFUNZI WA SHOOL YA MILLENIUM MWAKA 2010 WANAFUNZI WA SHULE HIO WALIKOPIA..NA NDIO ILIKUA YA 2 TANZANIA NZIMA HII STIRI KABLA YA RESULT HAZIJATOLEWA NI KUTOKA KWA MWANA S=FUNZI MWENYE AMBAYE ALIKATAA KUNDELEA NA SHULE HIO KWANI ALIONA NI KUJIDANGANYA
  NCHI NYINGI ZINAWEKA NAMBA KATIKA KUFANYA MITIHANI PAMOJA NA MATOKEO....NA RESULTS ZINAPOKWENDA MSHULE NDIO WANAZIWEKA KATIKA MAJINA
  SO WHATS THE BIG DEAL NECTA WASIFANYE HIVI
  MIMI SIAMINI KAMA SHULE MFANO PALE ALMUNTAZIR HAWANA AKILI...AMA HAWAPENDI KUSOMA..LAKINI NJAMA ZIPO....ILE SHULE MPAKA WAKAAMUA KUFANYA MITIHANI YA NJE YA CAMBRIDGE KWANI HAKUNA UADILIFU KUTOKA NECTA
  NA WANAFUNZI WENGI WANAFANYA VIZURI SANA NA WENGINE WAPO CANADA NA USA BAADA YA KUPATA SCHOLARSHIPS..LAKINI HII INGEKUWA NDOTO KAMA WALE WANGEFANYA NECTA.....
  NECTA IJISAFDISHE NA USIMAMIZI WA SHULE ZINAZIFABNYA VIZURI NAO UANGALIWE KWA KARIBU SIKU ZA MITIHANI ...

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...