Saturday, May 19, 2012

Ziara ya Joyous Celebration katika chuo kikuu cha Limpopo yawagusa wengi

Kiongozi wa kundi la Joyous Celebration  Jabu Hlongwane

Hivi karibuni Kundi la muziki wa injili kutoka Afrika ya kusini Joyous Celebration lilifanya ziara katika chuo kikuu cha Limpopo tawi la Mankweg nchini Afrika ya kusini. Ziara hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa kundi hilo kufanya katika chuo hicho, mara ya kwanza kundi hilo lilifika chuoni hapo  miaka mitano iliyopita.Wakiwa chuoni hapo Joyous walifanya huduma kwa takribani masaa sita mfululizo huku Charisma Hanekom, Uchechukwu Agu ama Uche wa Double Double na Mthunzi Namba wakikonga mioyo ya watu.

Wanafunzi wengi waliohudhuria huduma hiyo walisema wameridhika na performance ya kundi hilo na walikuwa wanatamani kundi hilo liendelee na hawakujutia pesa walizotumia kununulia tiketi kwa ajili ya onyesho hilo.Katika onyesho hilo Joyous walitumia nafasi hiyo kusisitiza kuwa kwa mwaka huu wataendesha zoezi la kusaka vipaji kwa wale wote wenye nia ya kujiunga na kundi hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...