Saturday, May 5, 2012

Kuteuliwa kwa Dr Mwakyembe kuwa waziri kamili, ni darasa lingine kwa kwanisa la TanzaniaDk Harrison Mwakyembe akishuka katika madhabahu ya Kanisa la Glory of Christ-Kawe mara baada ya kutoa shukrani kwa Mungu na ushuhuda kuhusu afya yake.


Biblia inasema njia za mwanadamu zikimpendeza Mungu, Mungu humpatanisha na adui zake, siku moja baada ya Rais Jakaya Mrisho kikwete kutangaza Baraza jipya la Mawaziri nchini Tanzania na kumtangaza Dr Haris Mwakyembe kama Waziri wa uchukuzi,kuteuliwa kwa Dr Mwakyembe kumetengeneza taswira pana kwa kanisa la Tanzania kwamba kutumia NAFASI uliyopewa na Mungu kwa ufasaha pamoja na Kumtanguliza Mungu katika nafasi hiyo huuvuta ukuu wa Mungu kuwa upande wako.

Rais Kikwete angeweza kumteua mtu mwingine kushika nafasi hiyo na kumwacha Dr Mwakyembe kwa kisingizio cha afya yake lakini laah,Rais amempa wizara kamili.

Ikumbukwe kuwa Dr Mwakyembe kabla ya kuwa waziri kamili alikuwa naibu waziri wa ujenzi akimsaidia Dr John Pombe Magufuli ambaye alikuwa ndiye Waziri wa wizara hiyo.Wakati akishikilia nafasi hiyo Dr Mwakyembe aliugua ugonjwa ambao mpaka leo haujulikani hasa ni nini kitendo ambacho kilimfanya kuwa nje ya wizara hiyo kimatibabu kwa zaidi ya  miezi sita.

Kinachogusa mioyo ya wengi hapa pamoja na kukaa kote huko nje ya ofisi, huku afya yake ikiripotiwa kuwa imeanza kuimarika leo hii Dr Mwakyembe kateuliwa kuwa Waziri kamili.

Mwaka huu Mwanzoni Dr Mwakyembe mara baada ya kurudi nchini kutokea India alikokuwa akitibiwa,alienda kutoa shukrani za pekee kwa Mungu katika kanisa la Glory of Christ Tanzania kanisa ambalo linaoongozwa na Mch Josephat Gwajima.Dr Mwakyembe anasifika sana kwa uadilifu wa kazi na majukumu yote anayopewa kitendo ambacho kimempa heshima ndani na nje ya chama chake cha Mapinduzi.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...