Tuesday, May 1, 2012

Kongamano kubwa la Wanawake kufanyika jijini Dar es salaamKongamano kubwa litakalowakutanisha wanawake wenye huduma tano pamoja na wake wa wachungaji , linatarajia kufanyika kwa siku tano mfululizo kuanzia tarehe 17-19/May/ 2012 katika ukumbi wa kanisa la Sinza Christian Centre jirani na kituo cha mabasi ya Sinza kumekucha kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na nusu jioni.

Pamoja na wke wa wachungaji, kongamano hilo liataweka pamoja wanawake wenye huduma tano za  kitume, Kinabii, Kichungaji, uinjilisti na ualimu.Kiongozi wa huduma ya Pastors wife Network Ministry (PAWINEM) ambayo imeandaa kongamano hilo mama askofu Haikaeli Shega amesema lengon la Kongamano hilo ni kuwasaidia wanawake wenye huduma kukabili changamoto kwenye huduma zao.
Waalimu watakaofundisha katika kongamano hilo ni

Askofu Joyce Nwanka kutoka Zambia
Mch Haikael Shegga
Mch Rahel Mwasota
Mch Imelda Maboya

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...