Monday, April 30, 2012

Magazeti ya Kikristo kwa ufupi




Kiti namba 666 katika Bunge la Ulaya chazua Balaa

Bunge la ulaya ambalo ndani yake kiti chenye namba 666 kiko wazi

 
Jengo kubwa la mnara wa Ajabu duniani unaosadikika kuwa mnara mwingine baada ya ule wa Baberi linalotumiwa na Bunge la Ulaya lililopo Brussels ubergiji, kwa muda mrefu sasa kiti namba 666 kati ya viti 778 vya wabunge wote wa bunge hilo hakina jina la mtu anayekikalia.Katika viti vyote 778 nina majina majina ya watu wanaovikalia.Mpango wa viti hivyo nadhifu uko nusu duara na viti vinavyokizunguka kti hicho na majina ya wanao vikalia ni kama ifuatavyo

663 Montfort
665Thomas Mauro
666 .............
667 Cappato
668 Turco

Katika mlango mkubwa wa kuingilia katika jengo hilo kuna sanamu kubwa ya mwanamke aliyepanda farasi akiwa nusu uchi.Uwazi wa kiti hicho umezua maswali mengi hasa kwa wachambuzi wa Biblia kutokana na Biblia kutamka wazi katika UFUNUO 13 kuwa namna 666 ni ya mpinga kristo.Wachambuzi wa Biblia wanasema umoja wa ulaya ni moja kati ya maeneo ambayo yanaharakisha ujio wa mpinga kristo.


Viongozi wa serikali na Dini wajadili Amani Tanzania

Viongozi wa serikali, dini, na taasisi mbalimbali nchini wiki iliyopita wamekutana kwa siku mbili ili kujadili mambo mbalimbali yatakayodumisha AMANI na Umoja wa watanzania.Mkutano huo ulifanyika katika Hotel ya White Sands ya jijini Dar es salaam na kufunguliwa na Makamu wa Rais Mh Mohamed Gharib Bilal ambaye aliwaasa viongozi wa didi kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza na kulinda umoja wan kitaifa na kusaidiana katika kukemea vitendo vya kifisadi.

Kwa mujibu wa Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of GOD(TAG) Askofu Barnabas Mtokambali ambaye alihudhuria kikao hicho alisema “ kikao hiki kimejenga msingi wa utatuzi wa matatizo ambayo yanaweza kuondoa Amani ya nchi yetu”

Mawaziri waonywa Ikimbieni hukumu ya Mungu
Mawaziri wenye tuhuma mbalimbali zinazowagusa wao binafsi au kushindwa kutekeleza wajibu wao na kusababisha uchungu na mateso makali kwa watu masikini na wale wenye kipato cha chini huku kukiwa na tishio la kutoweka kwa amani kutokana na kukithiri kwa tuhuma za ufdisadi na rushwa.

Wito huo umetolewa na viongozi wa dini na wabunge mbalimbali waliohojiwa na gazeti la jibu la Maisha katika nyakati tofauti tofauti.Akiongea kwa kujiamini Mbunge wa Iringa mjini Piter Msigwa alisema kuwa yeye alishiriki katika kamati ya bunge iliyokuwa ikichunguza tuhuma zilizokuwa zinamkabili waziri wa maliasili na utalii Mh Ezekiel Maige na alioyaona huko yanatisha kwa kuwa Mungu huwa na tabia ya kuchoka na kushusha hukumu yake kwa muhusika.

Msigwa ambaye pia ni Mchungaji alisema, nchi haiko salama kuliko unavyodhani, kwa kuwa kuna watu wengi walipaswa kufanya jambo kuliokoa taifa lakini bado hawajafanya. Wakati umefika kwa viongozi wa dini kujitenga na pesa zinazoletwa makanisani na watuhumiwa wa Ufisadi na tuwe makini kama nabii Mika kwa kuwaambia hapana.

Alisema kama viongozi wa dini wakisimama wakakataa wanasiasa mafisadi wanaojaribu kukimbilia kanisani kujisafisha kwa fedha chafu, wanachi hao wakisimama imara na kusema wizi, basi na wanasiasa wema waliosalia wakavunja nira na mafisadi nchi itasalimika.


Kutoka gazeti la Msemakweli

Pope Benedict
Mkuu wa wakatoriki duniani atangaza maisha yake kufikia ukingoni
Kiongozi wa kanisa katoriki duniani Papa Benedict XVI amesema kwamba hivi sasa anakaribia mwisho wa maisha yake katika umri wa miaka 85 alionao, lakini anauhakika kwamba Mungu atamsaidia katika kufanya kazi zake za Kitume.Kauli hiyo isiyotarajiwa imetolewa na kiongozi huyo wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa jijini Vatiokani nchini ITALIA yalipo makao makuu ya kanisa hilo duniani.

VCC Pastors fellowship kuandaa mkutano mkubwa jijini Dar es salaam
Huduma ya Pastors Fellowship inayoongozwa na kanisa la Victory Christian Centre  lililo chini ya Mch Huruma Nkone, limefanikiwa kutimiza maono yake baada ya kukusanya wachungaji mia tano wa mikoa ya Pwani na Dar es salaam.Ushirika huo wa wachungaji ulikutana katika ukumbi wa Hotel ya Landmark ya jijini Dar es salaam na moja kati ya mikakati yake ni kuandaa mkutano mkubwa utakaofanyika katika viwanja vya Jangwani mnamo mwezi sita mwaka huu wa 2012.


Gazeti la Nyakati

Mchungaji Masanja asema wanaoruhusu wanawake kuvaa suruari kanisani wamepotoka
Mchungaji Gervas Masanja wa kanisa la Pentekoste Mission Church la nchini Tanzania akiongea na Gazeti la Nyakati baada ya kuulizwa kama kuna tatizo lolote la kimaadili kwa mwanamke mkristo kuvaa suruali ibadani,Mch Masanja alijibu kama ifuatavyo “Kuvaa suruali kwa Mwanamke ni dhambi, Mapokeo na utandawazi vimewapoteza wengi, watumishi wanaowaruhusu waumini wao kuvaa suruali haijalishi ni kanisani au popote, hao sio watumishi wa Mungu mtu awe tayari kuwa na Bwana wakati wote. 

Wasabato masalia wataka waombwe radhi
Wachungaji watatu waliojitenga na kanisa la sabato(SDA) na kuanzisha kanisa linalojulikana kama Seventh Day Reformed  Remnants maarufu kama Wasabato Masalia wameutaka uongozi wa kanisa la SDA kuwaomba radhi vinginevyo watawapleka mahakamani..Hatua hii imekuja baada ya Kanisa la SDA kuwafungukia mashitaka viongozi wa masalia kwamba wamedurufu vitabu vya mwanzilishi wa kanisa la SDA Nabii Ellen White pasipo idhini ya Nabii 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...