Thursday, April 5, 2012

Nyimbo ya Kidum iitwayo YESU namba Moja

Kidumu

 Jean Pierre maarufu kama Kidumu ni Raia wa nchi ya Burundi ambako aliondoka nchini humo mwaka 1995  wakati wa machafuko na kuingia nchini Kenya ambako anaishi yeye na familia yake mpaka hivi leo. Kwa watu wanaomfahamu Kidumu wanatambua kwamba Jamaa ni mwanamuziki kwa kuwa tofauti na uwezo wake mkubwa wa kuimba, kidumu anao uwezo wa kupiga vyombo karibu vyote vya muziki, alianza kupiga Drumz akiwa na miaka kumi tu mnamo mwaka 1984.

Katika moja ya album yake ya Pili aliyoiita Ishano,Kidumu aliimba nyimbo ya Gospel iliyoshika chati sana nchini kenya na Burundi iitwayo "YESU NAMBA MOJA".Man of GOD soma hizo lyrics kisha angalia hiyo nyimbo naamini  utajifunza kwamba MUNGU ana kila aina ya watu wamtumikiao kwa namna tofauti tofauti kadri alivyowajalia.Artist: Kidum
Song: Namba Moja
Album: Ishano
Year: 2007
Producer: R Kay
Language: Kiswahili


Chorus
Nafasi yote moyoni nimeshaipa kwa Yesu
ni namba moja, moja moja, moja x 2


Verse 1
Nimeshatembea nimeshazunguka
kila pahali nikifika kila kona
nimejaribu kutafuta
kinachoweza kuridhisha moyo wangu
nikatanga tanga mashariki na kusini

ili muundaji nitafute nikamanga manga
magharibi kaskazini
kupata kile ninachotaka wimbo

Chorus
Nafasi yote moyoni nimeshaipa kwa Yesu
ni namba moja, moja moja, moja x 4


Verse 2
juhudi zangu zote zilipogonga mwamba
nikafa moyo nikakata tamaa
ndio bwana akaja kanigusa
nikasimama nikaanza kutembea
asante bwana mwokozi wangu

nimetambua kama nimekupata
pewa wimbo pewa sifa asante Yesu

Nimeshatembea nimeshazunguka
kila pahali nikifika kila korna
nimetambua nimekupata
Bwana Yesu mwokozi wangu nafasi

Chorus
Nafasi yote moyoni nimeshaipa kwa Yesu
ni namba moja, moja moja, moja x 4


1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...