Monday, April 2, 2012

Mtoto wa Mchungaji Joshua Nasari aibuka kidedea Arumeru Mashariki


Dr Wilbroad Slaa akiwa na Joshua Nasari wakati wa kampeni jimboni Arumeru Mashariki

Joshua Nasari ni mtoto wa tano kati ya watoto nane wa Mchungaji Samuel Nasari ambaye ni mchungaji wa kanisa dogo la Kiroho lililoko wilayani Arumeru.Hivi karibuni Joshua Nasari alikuwa akiiwakilisha Chama cha Demokrasia  na Maendeleo(CHADEMA) katika uchaguzi wa kuwania kiti cha Ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki uliomalizika siku ya jana na hatimaye Joshua kutangazwa Mshindi wa uchaguzi huo.

Katika Matokeo ya uchaguzi huo Joshua Nasari aliyezaliwa Mwaka 1985 alikuwa akipambana kwa ukaribu kabisa na mgombea wa kiti hicho kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Sioi Sumari.kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi, Joshua Nassari ameibuka mshindi baada ya kupata kura 32,972 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka CCM Bw. Sioi Sumari aliyepata kura 26,757.

Matokeo kwa Vyama vingine sita vilivyoshiriki ni kama ifuatavyo
DP -77 NRA - 35 AFP - 139 UPDB - 18 TLP - 18 SAU - 22

Kwa mujibu wa Bw. Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.

Joshua Nasari akiwa ameshikilia Biblia

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...