Diana Madida Kihayile |
Diana Madida Kihayile ni jina jipya baada ya kuolewa mwaka 2006 na Mr Bubele E
Kihayile.kabla ya hapo amekuwa akijulikana kwa jina la Diana Madida.Diana amezaliwa
na kukulia jijini Mwanza Tanzania,kwa sasa anaishi jijini Birmigham nchini
Uingereza.Yeye pamoja na mumewe Mungu amewajalia watoto wawili wa kike,Rina
Jodiah mwenye miaka miwili, na Jaina Sasha mwenye miaka mitano, kwa sasa Diana
pamoja na familia yake wanasali katika kanisa la El Shadai International
christian centre la jijini Birmigham nchini Uingereza.
Kimasomo Diana toka kidato cha kwanza mpaka cha sita amesomea shule ya sekondari Mwanza, wakati akiwa mdogo alikuwa anashiriki katika michezo ya utamaduni,ngonjera na kwaya ya shule.Pamoja na kushiriki kote huko lakini alikuwa bado ni mtu mwenye aibu nyingi japokuwa alikuwa anasikia furaha sana pindi akifanya kitu na watu wakafurahi.Ambition yake kubwa toka akiwa mdogo ilikua kuwa sister wa kanisani na mcheza netball.

Diana akiwa na mumuwe Bubere na mtoto wao |
Diana alimpa Yesu maisha mnamo june 1997
kupitia mkutano wa Dr Moses Kulola na kuanzia hapo akaamua kujiunga na kanisa
la E.AG.T IMANI lililo chini ya mchungaji Juliana Nyanda maeneo ya Pasiansi
jijini Mwanza napo ndipo safari yake kihuduma ilipoanza rasmi.Mwaka 1998,Diana
alijiunga na kwaya ya kanisa iitwayo FAITH AMBASSADORS ya kanisani kwao na baada
ya muda alianza kuimbisha baadhi ya nyimbo.
Mwaka 1999 aliendelea kukua kiroho
na kihuduma akaanza kulead ibada za kusifu na kuabudu ndani ya kanisa hilo na mwaka
2000 alijiunga rasmi na Kihayile band.
Mwaka 2003 alitoa
solo album aliyeipa jina la “MIMI NAJUA KWAMBA YESU ANANIPENDA” na ilisambazwa
na MAMU. Baada ya kutoa album hiyo mwaka uliofuatia yaani 2004 baada ya
kumaliza kidato cha sita Diana aliondoka
nchini na kuelekea jijini Birmingham kuendelea na masomo ya juu hivyo Mamu
hakuendelea tena kuisambaza album hiyo.
Diana on stage |
Alipofika nchini Birmingham
Diana aliendelea na huduma ya kusifu na kuabudu katika kanisa la Lighthouse
chapel. Mwaka 2008 kwa msaada wa Mumewe Mr. Bubele aliweza tena kutoa album ya
pili aliyoiita MILELE, album hiyo ilikuwa na nyimbo kama Uwe karibu nami,Tumeahidiwa
ufalme mwema na milele iliyobeba
jina la Album.Album hii Diana aliingiza sokoni nchini Uingereza na aliweza
kuituma nyumbani kwenye baadhi za vituo vya redio.
Baada ya hapo,Diana M Kiyahile aliweza kuunganisha plan zake kihuduma na mumewe ambapo ni jambo la kumshukuru Mungu kwani kwa mujibu wa Diana mwenyewe anasema “naamini mmoja anaweza ua elfu ila wawili makumi elfu.Mr bubele Kihayile is the perfect match from heaven to me,ni mentor wangu,mwalimu wangu,mtunzi wa nyimbo na muziki wote wa nyimbo zetu na mtumishi mwenzangu katika huduma”. Kwa sasa wana kihayire hao wanesharekodi nyimbo nne kati ya hizo wamerekodi video moja ya wimbo unaitwa Africa yetu.Kwa kipindi hiki Bubere na Diana wameanzisha huduma iitwayo Diana & Bubele Music ministries na kwa sasa wanaanda album ya kwanza ikiwa kama huduma kamili.
Marajio yao makubwa ni kuona ufalme wa Mungu umetukuka duniani na wanasisitiza “we are created to worship and to usher his people into his presence. Ni matarajio yetu kuongeza uamsho wa kusifu na kuabubu kwanza nyumbani kwetu Tanzania,Africa na duniani kote kwa ujumla,pia kwa kutumia muziki wa Africa kuleta uamsho ndani na nje ya afrika yetu.kwa kuwa Mungu ametupa instrument ambayo ni sauti na utunzi wetu tutaitumia kuyafanya mapenzi yake popote na kwa vyovyote atakavyo tuongoza,hatimaye tungependa tuwe mfano na daraja kwa watumishi wenye wito kama huu”
Mr and Mrs Bubere Kihayire |
Hosanna Inc: Ni Changamoto gani
ambazo mtu aliyeokoka anakutana nazo akiwa Uingereza ambazo asingeweza kuzikuta
akiwa Tanzania?
Diana:Mhh,kikubwa ni kubalance muda wa maisha kwa ujumla na
huduma,kwa hapa kila mtu yuko na wajibu wa kufanya kazi na kuedesha maisha yake
ambapo unakuta kila saa counts.Maisha ya UK kwa ujumla yanahitaji commitment
ambapo ili uweze kuwa sawa na kusurvive inabidi uwe na descpline ambapo ni
tofauti na Tanzania.Unaweza ukawa na muda wa kutosha kwenye huduma na maisha
yakaendelea kawaida,ila nisikufiche kwa hapa there is no chance ya kwenda
church five times a week! kama nilivyokuwa nafanya Tanzania.
Hosanna Inc: Artist gani wa injili ambaye kwa muda mrefu umekuwa ukimfatilia na amekuhamasisha sana katika kumtumikia Mungu?
Hosanna Inc: Artist gani wa injili ambaye kwa muda mrefu umekuwa ukimfatilia na amekuhamasisha sana katika kumtumikia Mungu?
Diana:Nimekua namsikiliza Cece winans kwani ni mwanamke ambaye
naamini ni kipenzi cha Mungu,anampresent Mungu katika uzuri na utukufu wake kwa
kina kinachoigusa mioyo ya wasiliklizaji wa nyimbo zake.Pia Yolanda adams ni
kiboko kwa kuitumia sauti yake kumtukuza Mungu.
Wito wake kwa kanisa la Tanzania
Ni vyema kuishi maisha yanayomwabudu Mungu,na kuedelea kuuboresha uhusiano wa mtu na Mungu mbali na huduma anayomfanyia Mungu,watumishi wengi wanasahau kuwa huduma sio uhusiano,pia inapokuja kwenye huduma wasidharau calling walizonazo na kutamani za wengine,kile Mungu alichomwekea mtumishi ndo portion yake na ukikitendea kazi Mungu atapanua hema yako na maisha yako yatakamilika.

White/Cream
Inaonyesha usafi na ni rahisi kuspot uchafu,pia
inapendeza.
Nje ya Huduma ya uimbaji Diana ni
Mwinjilist mwalimu wa watoto(suday school)
What is ur Favourite Gospel Song kwa Tanzania
Unajibu maombi-Upendo Kilahiro
What is ur Favourite Gospel Song kwa Tanzania
Unajibu maombi-Upendo Kilahiro
Her Favourite Gospel Song nje ya Tanzania
My redeemer lives (Nicole C Mullins)
What is your Favourite Gospel Hym{Tenzi}
Bwana Mungu nashangaa kabisa .
Her Favourite Bible verse
Mathew 7:7
What is your Favourite Gospel Hym{Tenzi}
Bwana Mungu nashangaa kabisa .
Her Favourite Bible verse
Mathew 7:7
Ombeni nanyi mtapewa,tafuteni nanyi mtaona,bisheni
nanyi mtafunguliwa,
God has been faithful to me tangu nimeokoka nimeusimamia huu mstari na ninaendelea kuona matunda makuuubwa sana.
God has been faithful to me tangu nimeokoka nimeusimamia huu mstari na ninaendelea kuona matunda makuuubwa sana.
MUNGU AWABARIKI HAWA WATUMISHI WA MUNGU KAZI YAO KTK BWANA SIO BURE WATALIPWA NA BWANA,ASANTE KWA INFO.UBARIKIWE
ReplyDelete