Monday, April 9, 2012

Tamasha la Pasaka 2012 lawagusa wengi



Siku ya Jana katika uwanja mpya wa Taifa kulifanyika Tamasha la Pasaka ambapo wanamuziki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi walipanda madhabahuni kwa lengo la kumsifu na kumwabudu Mungu.Katika tamasha hilo  lililohudhuriwa na watu wengi maaarufu ampapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Benard Membe.Tofauti na Membe alikuwepo pia Askofu Silvester Gamanywa,Balozi wa Zambia nchini,Pamoja  na Nape Nauye

Katika Tamasha hilo waimbaji wengi walipanda jukwaani akiwemo Upendo Kilahiro. Upendo Nkone, Solomon Mukubwa,Emmy Kosgei,Rose Muhando,Anastazia Mukabwa, Ephraim Sekeleti,Glorious Celebration, Kinondoni Revival Choir, pamoja na Rebecca Malope.

Solomon Mukubwa ni mmoja kati ya waimbaji ambao walifanya Vizuri siku ya janakwa kuimba LIVE huku akiwa na timu yake nzima kuanzia watu wakum-back up pamoja na wapigaji.Alianza kuimba nyimbo yake ya MUNGU MWENYE NGUVU wimbo ambao ulipelekea uwanja mzima kulipuka kwa furaha kisha akaimba wimbo wake mpya uliobeba album uitwao UTUKUFU WOTE.Wimbo huu wa UTUKUFU WOTE ni mpya na unapatikana katika Album yake iliypewa jina la nyimbo hiyo. Na ilizinduliwa Jana na Mhe Bernard Membe.

Ephraim Sekeleti Mutharange  alipanda madhabahuni akiwa amevalia suruali ya kadet nyeusi,shati jesusi pamoja na Koti la suti la Brown huku akiwa na mpiga gitaa maarufu nchini Sam Yona, Sekeleti huku akipiga Keyboard na alianza kuimba wimbo wake wa Uniongoze uliopelekea uwanja mzima kuimba naye. Baada ya wimbo huo aliimba wimbo wake mpya uitwao Mungu Hajalala ambao kikweli unagusa Moyo wa Mungu

Rose Muhandounaweza msema na kumjudge vyovyote lakini kwa habari ya Kumiliki stage Mungu ameweka kitu kikubwa ndani yake.Akiwa na timu yake ni mwanamuziki aliyesababisha uwanja mzima kusimama kuanzia alipoimba wimbo wake wa  kwanza mpaka alipomalizia na wimbo wake wa pili wa Utamu wa Yesu.Rose alionyesha uwezo mkubwa(uwezo binafsi) wa kuimba huku akicheza na kuishirikisha hadhira.

Baada ya Rose ndipo alipopanda jukwaani Malkia wa Muziki wa injili Barani Afrika Rebecca Malope.Baada ya kuimba wimbo wake wa Moyo wami Rebecca alisema amesikitishwa na kifo cha Steven Kanumba na amekumbuka kifo cha wadogo zake mapacha wawili.Rebeka akiwa na timu yake kuanzia waimbaji mpaka wapigaji alimba nyimbo takribani tano kasha aliwaaga mashabiki na kuahidi akirudi nchini anampango wa kununua nyimba nchini Tanzania.

Rose Muhando na Emmy Kosgei wakiingia uwanjani

Waziri Membe akizindua Album Mpya Ya Solomon Mukubwa iitwayo Utukufu ni Wako
Glorious Celebration on stage
Hadson Kamoga akiwa na Sekeleti

John Lisu on stage

Mtume Fernandes akiwa na Bernard Membe

Sehemu ya Umati uliokuwepo

Rebecca Malope on stage

Ephrai Sekeleti on stage

1 comment:

  1. Safi sana tamasha la pasaka. linanipa changamoto ya kujituma zaidi katika kazi ya kumtumikia Mungu kupitia Uimbaji

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...