Monday, April 16, 2012

Kanumba alipuuza unabii wa kifo chake


Steven kanumba
Kifo cha msanii mahiri wa maigizo nchini Steven kanumba ambaye alizikwa jumanne iliyopita katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam kimeelezwa pengine kuwa kisingetokea endapo angekubali kukutana na mwimbaji wa injili asiyefahamika sana Dorice Mkangama ambaye anasema Mungu alimpa maono ya Kifo cha Kanumba.

Siku moja baada ya kifo cha Kanumba Dorice alikutana na mwandishi wa gazeti la Nyakati, linaloandika habari za kikristo nchini siku ya Pasaka katika kanisa la la Amri Kumi Za Mungu(AKUZAMU).Baada ya kukutana Dorice aliweleza mwandishi kuwa Kanumba alikuwa amezingirwa na pepo la mauti, na kwa bahati mbaya licha ya kufanya jitihada za kukutana naye ili alishughulikie pepo hilo kwa maombi, kuna nguvu nyingine ilikwamisha mpango huo wa Kiroho.

Huku akimuonyesha mwandishi nakala ya barua aliyomwandikia Kanumba kumuomba akutane naye , ambayo imesainiwa na na kupokelewa na sekretari wa kanumba ajulikanaye kwa jina la Gisela, Dorice anasema baada ya kuonyeshwa na Mungu juu ya kifo cha Kanumba alijitahidi akutane naye ili ampe Kanumba huduma za Kiroho lakini hakufanikiwa.

Mtumishi huyo alizidi kumwambia mwandishi wa Nyakati kuwa “Niliona maono ya kifo chake, kweli kaka nikaanza kumfatilia. Nilienda Mwenge ambako niliambia anafanyia shughuli zake nikaambiwa amehamia Sinza Maeda.Nikapiga mguu mpaka Sinza Maeda ofisini kwake.Nilipofika nikawakuta watu wake baadaye niliambiwa kwa majina kuwa  wanaitwa Gisela na mwingine anaitwa Magulu, niliwaambia kuwa naomba nionane na Kanumba, sijui walinichukuliaje wakanambia kuwa siwezi onana na Kanumba”

Nilishangaa hawakuniruhusu kabisa kukutata naye sijui walifikiri nataka kumtongoza, baaaya waliniambia niandike barua.Siku hiyo hiyo nikaandika barua, na ili asinione mimi ni wa barabarani tu kwenye barua nikaweka wadhamini wangu ambao ni Pritesh wa Steps Entetainment wasambazaji wa kazi za filamu nchini, pamoja na mchungaji wangu Gwandu Mwangasa.

Kwa kawaida nisingeweza kumwambia mambo hayo kwa haraka haraka, ila ningeombea Roho ya mauti iliyokuwa ikimfatilia na Mungu angemnusuru na kifo alisema Dorice Mkangama ambaye ni muumini wa kanisa la Glory of Christ church Tanzania maarufu kama nyumba ya Ufufuo na Uzima inayoongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima.

Dorice anasema alishaonyeshwa vifo vya watu wengi nikaaombea sasa wako hai hadi leo,Dorice anauhakika kwa Neema ya Mungu kama angeonana na Kanumba basi kanumba asingefariki.Dorice aliandika barua hiyo tarehe 3/04/2012 na kuikabidhi siki hiyo hiyo na Kanumba alifariki usiku wa kuamkia tarehe 7/04/2012.


Ninachokuambia Mwandishi  ni kwamba kifo cha Kanumba ni Pre-Mature death, kuna watu wanakaa kwenye vyumba mahututi hospitalini(ICU) siku nyingi lakini hawafi, Kanumba kafa Kirahisi mno.Nilipoonyshwa Kifo cha Kanumba kuna watumishi niliwashirikisha mfano ni Mtume Marko Biganyeka na huyu ndiye aliyenitumia ujumbe wa simu kuwa Kanumba kafariki alisema Dorice Mkangama

Source:Nyakati

6 comments:

 1. DUU KUMBE HAPA SI BWANA ALIYETWAA KAMA TUNAVYOJIFARIJI.................

  ReplyDelete
 2. mm nakulaumu sana ww dorice.Ulitakiwa uombe kibali toka kwa Mwenyezi mungu cha kuonana na Kanumba wala sio kwa secretary wake.Ulionyeshwa hili ili uliepushe Kwa kukemea.Au unafikiri mungu ana maana gani kukuonyeshaa?

  ReplyDelete
 3. uko sawa anonymous

  ReplyDelete
 4. Nafikiri kama mtumishi wa Mungu ingefaa huyu dada Dorice amuombee haikuwa lazima kuonana naye kwani Mungu akikuonyesha kitu kama mtumishi wake yafaa uombe sana tena kwa mzigo kwa kuwa unamuombea mtu asiyeokoka lazima ujinyime uwe katika nafasi yake, kwanza umuombee rehema kisha umuombee Mungu amuepushe na hayo mauti. samahani lakini hayo ndio maoni yangu kama mkristo.

  ReplyDelete
 5. NAKUBALIANA NA WEWE KABISA MUNGU ANAPOTUONESHA VITU HAIMAAMINISHI NI LAZIMA TUWE KARIBU NA WATU AMBAO TUNAHITAJIKA KUWAOMBEA KWASABABU TUMEPEWA MAMLAKA YA KUTAWALA NA KUMILIKI KWA NJIA YA MOMB AMBAYO INATUWEZESHESHA KUWA KARIBU KIROH NA MTU TUNAYEMUOMBEA HATA KAMA HAJUI KAMA TUNAMUOMBEA...HIVYO NADANI DORICE BADO ALIKUWA NA UWEZO KABISA WA KULIZUIA HILO...

  ReplyDelete
 6. jamani msimlaumusana dada Dorice, huwezi jua labda pengine Mungu alimtuma akaonane nae uso kwa uso kwa sababu kuna mapepo mengine huwa hayatoki mpaka umuombee huyo mwenye pepo kwa kushika either kichwani au kifuani au mgongoni ndipo pepo liweze kutoka

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...