Wednesday, April 11, 2012

Mungu akisema na wewe,Usipomuelewa, Muulize - Danstan Haule Maboya


Apostle Danstan Maboya
Katika utumishi, usiangalie mazingira uliyopo, Muangalie yeye aliyekuita.

Tukijenga tabia ya kumuheshimu Mungu, na sifa zake zikabaki palepale pasipo kuzichukua, tutafufua maiti.


Waamuzi 6:11-15

Mara nyingi Mungu akitaka kufanya jambo husema na mtu ama watu, anapokuja kusema na wewe kisha usiuelewe ujumbe huo usiseme ndio nimesikia Bwana,Muulize ili akufafanulie kwa kuwa yeye ni Baba yetu na anatupenda.Biblia inasema (Waamuzi 6:11-15) baada ya malaika wa Bwana kumtokea GIDEON alimpa Gideon sifa nyingi,kuwa wewe ni shujaa,Roho wa Bwana yu juu yako.


Hata kama Mungu ataongea na wewe, usipomuelewa ni lazima umuombe aongee lugha rahisi ambayo utaielewa, watu wote ambao wako sharp huwa hawapokei ujumbe ambao haueleweki, huuliza!!.Kuna wakati Mungu huongea lugha ngumu mfano alipoandika MENE MENE TEKELI NA PELESI.Lugha hii haikuwa nyepesi kwa mfalme Belshaza ndipo Belshaza akatafuta tafsiri kwa waganga  na wazee wakashindwa, ila alipokuja Daniel ile kusoma tu, akajua hii ni Lugha ya Mbinguni akatoa tafsiri.

Gideon baada ya kupewa sifa zote hizo akasema “tulia”,hivyo vyeo ni vingi mno utaniitaje kuwa mimi ni shujaa wakati familia yangu na hali yangu ni duni?.Alijiuliza utaniitaje shujaa wakati watu wangu wanataabika, utaniitaje shujaa wakati mazingira yangu ni mabaya. Pongezi na sifa alizopewa na Mungu kwake hakuzielewa.

Zaidi ya hapo Kitendo cha Mungu kumwambia Gideon “amka wewe uliye shujaa” haikuwa lugha nyepesi kwa Gideon kwa kuwa katika Makabila yote 12 ya Israel kila kabila Mungu alilipa Majukumu, kabila la walawi wao walikuwa wakiongoza shughuli zote za Kuabudu, wakati kabila la Yuda wao walikuwa wamepewa kufanya shughuli zote za uongozi(Administration), na makabila mengine yakapewa shughuli nyingine.Gideon hakutoka Ukoo wa Lawi wala wa Yuda, Gideon alitoka ukoo Kabila la Manase ambalo wao walionekana dhaifu hivyo halikuwa jambo la kawaida.

Ni kama wewe leo unajiangalia ulivyo, ukiangalia familia yako huko nyuma  wote wanaabudu mizimu na kwenda kwa waganga wa kienyeji, katikati ya hali hiyo unakuta yupo mtoto ananena kwa Lugha. kwa habari ya Gideon Mungu hakuangalia Mazingira aliangalia Roho, akamwita Gideon shujaa kwa kuwa kipindi hicho Makabila yote ya Israel yalikuwa yamevulugikiwa.

Tumezoea kuona kama baba akiwa jambazi itaenda hiyo hali kwa watoto mpaka wajukuu, vivyo hivyo kwa makuhani,ilikuwa ni desturi kama baba ni kuhani utakuta mpaka watoto ni makuhani.Ezekiel 18:20 Biblia inasema “ROHO ITENDAYO DHAMBI, NDIYO ITAKAYO KUFA”.Ukijipanga vizuri na Mungu haijalishi familia yako ikoje unaweza ku-change destiny ya familia yako.Wakati Gideon anauliza yeye alikuwa bado yuko katika mazingira ya kawaida hakujua nini Mungu anaangalia.Katika utumishi, usiangalie mazingira uliyopo, Muangalie yeye aliyekuita.

Tukijenga tabia ya kumuheshimu Mungu, na sifa zake zikabaki palepale pasipo kuzichukua, tutafufua maiti.Wakati mwingine Mungu anashindwa kutenda  mambo makubwa kwetu na kutuachia madogo, kwa kuwa anajua vichwa vyetu haviwezi kubeba.Mungu aliona kitu cha Tofauti kwa Gideon ndipo akaamua kuwaacha waisrael  wote na kumtumia Gideon.

Gideon alipoona hamuelewi Mungu aliomba Mungu afanye ishara ili kulithibitisha neno lake(Waamuzi 6:17), Mungu kupitia malaika alimjibu Gideon kwa kufanya ishara.


Apostle Danstan Haule Maboya

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...