Wednesday, April 18, 2012

Sonnie Badu - Mwanamuziki Bora wa Injili Barani Afrika 2010/2011

Sonnie Badu

Sonnie Badu ni Mwanamuziki wa injili kutoka nchini Ghana, kwa muda mrefu sasa Sonnie amekuwa akihudumu nchini Uingereza.Kwa watu wanaomfahamu na kumfatilia sonnie kiasili ni Worshiper.Akiwa madhabahuni akiimba nyimbo yake ya “Convenat keeping God” mama mmoja mwenye kansa na mwingine alikuwa mgumba waliponywa na Kristo matatizo yao.

Sonnie Badu alichaguliwa mwaka jana kuwa mwanamuziki Bora wa nyimbo za Injili barani Afrika nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Ucheagu(My God is Good oooh-Double Double) kwa miaka miwili mfululizo.Hapa chini ni nyimbo yake iitwayo BABA ambayo kimsingi imemtambulisha vilivyo Mtumishi huyu.Tofauti na ubora wa nyimbo yenyewe katika video hii, kuna darasa huru kwa ma-director wa video za injili nchini.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...