Monday, April 9, 2012

Godbless Lema alitangaza kuanza maombi ya kufunga na kuombaGodbless Lema
Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Mh Godbless Lema  juzi, alitangaza kuanza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku saba kuanzia jumatano ya tarehe 11 April 2012 na kuomba kila mwananchi anayependa haki kwa imani yake kumuunga mkono katika maombi hayo ya kufunga na kuomba. Pia aliomba maombi hayo yaendane na kuwasaidia maskini na wajane na wale wasiojiweza kwa vile vitu ambavyo Mungu ametubariki kwavyo.

Lengo kuu la maombi hayo ni kumuomba Mungu aingilie kati na kulipiza kisasi kwa wale ambao wametumia nafasi zao kushinikiza hukumu isiyo ya haki ambayo ilitolewa hivi karibuni na kumfanya aende likizo katika nafasi yake ya ubunge na pia maombi ya shukrani kwa Mungu kwa yote yaliyotokea.Hayo aliyasema juzi katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya NMC jijini Arusha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...