† Huwezi
kutawala mwili pasipo Roho,Roho ndiyo inatawala mwili, ulimwengu wa Roho ndiyo
ulioumbwa kwanza na ulimwengu wa mwili ukafyatuliwa,kutoka ulimwengu wa Roho.
† Baba anasema tufanye mtu, Mwana anakwenda kufanya mtu, ni
Roho Mtakatifu anayekwenda kudhihirisha ule udongo wa tope unakuwa mwili, nyama,damu
na mifupa mtu anakuwa nafsi hai. Ni baba anayesema mguse kipofu, ni Yesu
anayemgusa kipofu , ni Roho mtakatifu anayerudisha golori kwenye macho ya
kipofu.
Mwl Mgisa Mtebe
|
Rumi 8 :29
Usijilinganishe na
mtu mwingine yeyote,jilinganishe na Kristo tafuta kufanana na Yesu, si sawa
kabisa kujazwa na Roho Mtakatifu kisha ukawa mtu wa kawaida,
Kanuni za kawaida
kabisa zikikugomea lile gape la tarajio
na uhalisia linapokuja unafanya nini, ulikuwa unatarajia hiki kikaja hiki kuna
gape hapo,hapo ndipo unaingiza kitu kinaitwa gia ya Imani, unaaply the
supernatural kwa kuwa NATURE imeku-dissapoint.Ulitegemea ukisoma utafaulu
lakini kadri unavyoendelea kusoma matokeo yanazidi kuwa mabaya kuna gape hapo
kati ya kusoma na matarajio.Sasa unalijazaje hilo gape hapo kati ya tarajio na
hali halisi.Wewe umeokoka hutakiwi kuiba mitihani wala kuibia ukiwa katika
chumba cha mitihani ili na baadaye uende mbinguni vile vile, usije ukapata
“A”ukaenda jehanum.Palipo na gape kati ya tarajio na uhalisia ndipo gia ya
imani huingia.
Kuna namna mtoto wa
Mungu anaweza akaishi duniani bila kujichafua na akapingana na changamoto zote za maisha ya kikristo na
akashinda, akawa succsesfull duniani na mbinguni akaingia.Kuna kanuni zake,
pale maisha yanapokuwekea gape ndipo unaingiza gia ya Imani. Kuna vitu vingi
vinachangia katika uwezo wa mtu wa kiakili, kitaalamu intellingent quotient(IQ).
Unataka kufaulu unataka kukumbuka, unakuta unaomba na unalala darasani kisha
haufaulu, lakini wapo ambao kabla ya kwenda kusoma wanaenda vuta bangi.Matokeo
yakija wao manapata A na wewe unapata ”C” wakati na kunena kwa lugha unanena.
Tatizo la kiakili
sio lazima liwe limechangiwa na mapepo, kitaalamu wataalamu wa saikolojia
wanasema wakati baba yako na mama yako wanakutafuta walikuwa katika hali gani,
kama walikuwa mawekasilishana, wanawaza madeni na matatizo, vile vichembechembe
vinatengeneza makeup ya wewe baadaye, na hata wakati umetungwa mimba mama yako alikuwa
katika hali gani, kama alikuwa mtu wa machozi,kukasirika, kulalamika hivyo
vichembechembe viliingia, na alikuwa anakula chakula gani hilo nalo ni la
msingi.
Na hata wakati
unazaliwa ulikaa sekunde ngapi ukikosa hewa, kama ulikaa muda mrefu pasipo kuvuta
hewa, uwezo wa kiakili hushuka.Hapo utaona uwezo wa kiakili hauchangiwi tu na
mambo ya kiroho.Haya sasa umeshazaliwa katika mazingira hayo na uko first year
unafaulu vipi? Ukijikuta katika hali hiyo ya kimasomo hapo ndipo Imani
hutumika, wakati wengine wanatarajia ufeli lakini kwa imani unalijaza hilo gape
na kufaulu
Unamawazo ya kuwa
Lawyer, Accountant, daktari anakwambia moyo wako umechoka,au anasema una kansa
ya damu,umetarajia biashara itaenda hivi inaenda hivi, maisha yanakufrastrate
yanakutendea visivyo.Hapo ndipo NGUVU ya imani inapoingia kazini,kila mtu anaye
kujua kiuchumi, kiakili anashangaa umefika vipi upande wa pili na umewaacha
watu wote midomo wazi.
Yesu aliposema
nyumba iliyojengwa juu ya mawe alimaanisha nini,yale mawe hayahitajiki siku zote
yanahitajika siku ya Dhoruba na siku ya tetemeko,dhoruba isipokuja tetemeko
lisipokuja aliyejenga juu ya mawe na juu ya mchanga hakuna tofauti,the only
defference ni siku ya disaster.
Wakati wengine
wanafaulu hali kwako inakuwa ngumu, usione kuwa kuendelea kusali ni kitu kama
mzigo vile, wee endelea kuwekeza kwa kuwa kuna siku ya dhoruba.Tunajifunza haya
mambo ili tuweze kupata kila kitu ambacho Mungu alitukusudia cha
kutuwezesha kuishi maisha ya ushindi na
mafanikio duniani. Hatukuitwa kuteseka, hatukuitwa kushindwa, kufeli
kuhangaika.Huwezi kufanikiwa katika ulimwengu huu pasipo kutumia nguvu fulani
ya Kiroho.
Huwezi kutawala
mwili pasipo Roho,Roho ndiyo inatawala mwili, ulimwengu wa Roho ndiyo ulioumbwa
kwanza na ulimwengu wa mwili ukafyatuliwa/ ukazaliwa kutoka ulimwengu wa Roho.Sio kwamba ulimwengu
wa Roho uliumbwa kushoto ulimwengu wa mwili ukaumbwa kulia, ulimwengu wa Roho
uliumbwa kwanza ulipokamilika
vilivyokuwa ndani ya ulimwengu wa Roho vikazaa ulimwengu wa mwili.
Hivyo ulimwengu wa
mwili umetokea katika ulimwengu wa Roho,huwezi kutawala ulimwengu wa mwili,
bila kupitia nguvu ya kiroho.Unahitaji nguvu za MUNGU,na Roho mtakatifu ndiye
NGUVU YA MUNGU, ndiye anayewezesha kauli ya Baba na matendo ya mwana yanakuwa
dhahiri. Baba anasema tufanye mtu, Mwana anakwenda kufanya mtu, ni Roho
Mtakatifu anayekwenda kudhihirisha ule udongo wa tope unakuwa mwili nyama damu
na mifupa mtu anakuwa nafsi hai. Ni baba anayesema mguse kipofu, ni Yesu anayemgusa
kipofu, ni Roho mtakatifu anayerudisha golori kwenye macho ya kipofu.
Kwa kupewa Roho
mtakatifu ni kukufanya uwe kama Yesu,kwa kuwa anakuambukiza uwezo aliokuwa nao
Yesu. 1Yoh 4: 12-17 “Kama yeye alivyo na
sisi ndivyo Tulivyo” Rum 8: 29, Efeso 4; 11-14.Mungu anataka uwe YESU Mdogo
duniani, ufananishwe na mfano wa mwanawe, watu wote wanaomhitaji Yesu waje
kwako kwa kuwa yeye alivyo ni kama wewe kwa kuwa umepewa Roho wake.
Itaendelea......
Mwl Mgisa Mtebe
No comments:
Post a Comment