Tuesday, April 10, 2012

Pastor Zakayo Nzogele katika Ibada nchini Korea Kusini

Wakorea wakiwa mbele za uso wa Mungu

Mchungaji Zakayo Nzogele ni mtumishi wa Mungu na mchungaji kiongozi wa Kanisa la Mwanza International Christian Centre(MICC). Kwa sasa yeye na Familia yake wako Masomoni chini Korea kusini.Wakati Pastor Zakayo akichukua masomo yake ya shahada ya Uzamili(Masters ) na kisha ataendelea na ile ya Uzamivu(Ph D), Mama Mchungaji Zakayo yeye anachukua Shahada ya Kwanza.

Tofauti na Masomo Pastor Zakayo ni mchungaji msaidizi wa kanisa la Youngnak Church-IWE(Intenatonal Worship) lililoko nchini humo.Hosanna Inc ilipotaka kujua nini hatima yake na nchi yetu, Pastor Zakayo alisema ingawa yuko nchini humo yeye na Familia yake pamoja na watoto wake wawili LAZIMA ATARUDI NCHINI mara baada ya Masomo, na kamwe hawezi kutokomea.Tofauti na kuchunga kondoo wa Bwana, Mch Nzogele ni Muimbaji, na hupiga vyombo vya muziki karibu vyote

Hapa chini Pastor Nzogele akiimba katika Ibada ya Ijumaa kuu nchini Korea Kusini

Wa kwanza kulia ni Pastor Zakayo Nzogele

Pastor Zakayo Nzogele akiabudu katika ibada ya Ijumaa kuu

Sehemu ya Umati uliohudhuria ibada hiyo

Praising going on
Wakorea wakiwa mbele za uso wa Mungu

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...