Mwanamuziki
wa Injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekeleti, jumapili ya leo tarehe
14/04/2012 alihudumu katika ibada kwenye kanisa la Living Water Kawe
Makuti.Katika ibada hiyo Sekeleti aliimba nyimbo zake maarufu ikiwemo Uniongoze
pamoja na nyimbo zake nyingine zilizomo kwenye album yake mpya iitwayo Acha
Kulia.
Katika
hali iliyoonekana kuvuta hisia za wengi kanisani hapo, ni pale mtumishi huyo
ambaye ni baba wa watoto wawili alipotoa ushuhuda wa maisha yake kwa ufupi,
ambapo hadi anamaliza kuusimulia watu wengi walikuwa wakilia kwa namna ambavyo
Mungu alimtetea mtumishi huyo katika Maisha yake toka anazaliwa mpaka hivi leo.
Katika
ushuhuda huo kwa kifupi sekeleti alisema akiwa mdogo alipata ugonjwa uliosumbua
maeneo ya shingo na mdomoni, yeye pamoja na familia yake walisumbuka sana
kupata matibabu, walienda sehemu zote lakini hawakupata msaada.Ilifikia hatua
walienda mpaka kwa waganga wa kienyeji lakini hawakupata msaada.
Katika
haali hiyo ndipo Ephraim aliweka Agano na Mungu kuwa endapo Mungu utaniponya
basi nitakutumikia katika maisha yangu yote.Kwa kuwa Mungu ni mwenye nguvu
alimponya Ephraim na ndipo kuanzia hapo Ephraim Sekeleti alianza kumtumikia
Mungu. Mpaka sasa Sekeleti ana jumla ya album zipatazo saba ambazo ameziimba
kwa Lugha za Ki-bemba,Ki-nyanja,Kiingereza na Kiswahili.
No comments:
Post a Comment