Thursday, April 12, 2012

Kufuatia Kifo cha Rais Bingu Mutharika wa Malawi,Wengi wazidi Kumwamini Phrophet TB Joshua

Amefariki ndani ya Miezi miwili aliyosema Nabii TB Joshua

Baada ya unabii wa Tb Joshua Wazimbabwe na wamalawi waliamini TB Joshua alikuwa akitabiri juu ya marais wao.

Heshima ya TB Joshua yaongezeka Maradufu


Rais wa Malawi Bingu Mutharika(78) aliyefariki alhamis iliyopita baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo, amekuwa ni Rais wa kwanza kufariki siku za hivi karibuni  kati ya mlolongo wa Marais wengi wazee walioko madarakani barani Afrika, ambao kwa namna moja au nyingine unabii wa Nabii TB Joshua ulikuwa ukiyagusa maisha yao.

Mtumishi wa Mungu TB Joshua
Mnamo tarehe 5-02-2012 Mtumishi wa Mungu TB Joshua akiwa katika moja ya ibada za jumapili katika kanisa lake alisikika akisema “ Tuombe,Naona kifo cha ghafla kwa rais mmoja mzee(mwenye umri mkubwa) wa bara la Afrika ndani ya miezi miwili ijayo”.
 
Kitendo cha Rais Mutharika kuiaga dunia mnamo tarehe 6-04-2012,Kwa hesabu za haraka haraka utaweza kuona kifo cha ghafla cha rais Mutharika kimetokea ndani ya siku sitini na moja(miezi miwili) ya unabii aliosema mtumishi wa Mungu Temitope Joshua.

Pamoja na hayo Jumapili iliyopita  ya tarehe 01.04.2012 akiwa kanisani kwake,  nabii TB Joshua alisema tena na hapa namnukuu “I was talking about April, we should pray for the nation, this country… God loves us, you should pray for one African head of state, when I say President… again the sickness that is likely to take life; sudden death.”

Kufuatia kifo cha Mutharika mamia ya watu ulimwenguni waliokuwa wakimpiga na kuwa na mashaka juu ya huduma na mwenendo mzima wa huduma ya TB Joshua, kwa sasa wameonyesha kumkubali kuwa ni NABII WA MUNGU.

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Malawi Marehemu Bingu Mutharika
 
Ikumbukwe kwamba mara baada ya  unabi wa TB Joshua kutoka, mamia ya Raia Zimbabwe walianzisha Mijadala kwenye mitandao Jamii wakiuhusisha unabii huo na Uhai wa Rais wao Mh Robert Mugabe.Naye msemaji wa chama Tawala cha nchi hiyo Mh Mh Rugare Gumbo yeye alipoulizwa juu ya utabiri huo alisema “I do not believe some of these prophecies of doom,”

Nchini Malawi wengi wa raia wa nchi hiyo waliamini kuwa unabii wa Tb Joshua kwa kiasi kikubwa uliyahusu maisha ya Rais wao Mh Mutharika, na hii ni kutokana na umri wake pamoja na afya yake ambayo kwa muda mrefu ilikuwa sio nzuri.

Miongoni mwa Marais wenye umri mrefu walioko Madarakani barani Afrika na ambao kwa namna moja au nyingine walikuwa wakiguswa na unabii huo  ni pamoja na


Rais wa Senegal Mh Abdoulaye Wade mwenye miaka 85
Rais wa Kenya Mh Mwai Kibaki mwenye umri wa miaka 81.
Rais wa Cameroon Mh Paul Biya mwenye umri wa miaka 79,
Rais wa Zambia Mh Sata yeye anaumri wa miaka 79


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...