Tuesday, April 10, 2012

Marehemu Steven Kanumba alipania kurekodi album ya Muziki wa Injili


Steven Kanumba
 Wakati Tanzania ikiomboleza mazishi ya Msanii wa Filamu maarufu nchini Tha Great Steven Charles Kanumba, imefahamika kwamba kabla ya kifo chake marehemu alikuwa na mpango wa kurekodi album ya muziki wa injili na tayari alikuwa amesharekodi nyimbo takribani tatu. Kati ya nyimbo hizo, nyimbo moja inaitwa Nitayainua macho yangu ambayo tofauti na kuimba amepiga mwenyewe gitaa la base.

Nyimbo nyingine inahusu Harusi, Steven kanumba alipania sana kuiimba nyimbo hiyo siku ya harusi yake na hii ni kwa mujibu wa mmoja wa marafiki zake wa karibu. Leo tarehe 10/04/2012 ni Mazishi ya kijana huyu aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa tasnia ya Filamu nchini.Marehemu kanumba atazikwa leo katika makaburi ya kinondoni na mwili wake utaagwa katika viwanja vya leaders Club kuanzia saa tatu asubuhi.Bwana ametoa, na bwana ametwaa, jina lake libarikiwe.

Yafuatayo ni baadhi ya Maneno yaliyomo katika wimbo wa Marehemu Steven Kanumba uitwao “Nitayainua Macho yangu nitazame Milima” 

Kama leo nikifa kila mtu atanisifu kwa lake,
hata hao wanaonichukia watabeba jeneza langu,
kwa nyimbo na sala za uzuni,
Mwenzangu leo niko hai twachukiana sana ,
usoni wa cheka rohoni ni vita,
Tusameane tuishi kwa upendo na amani,
Furaha yetu hadi mbinguni tuwe na furaha ya milele.


Hadi jana jioni Maandalizi ya Mazishi yake yalikuwa yanaendelea katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni

Mazingira yakiwekwa safi

Stage ya kumuagia Tha Great ikiwa katika hatua za Mwisho

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...