Tuesday, April 17, 2012

Familia ya Askofu David Oyedepo

Familia ya Askofu David Oyedepo na jamaa zao, wenye nyeupe katikati ni Pastor Isaack Oyedepo na mkewe, wa kwanza kulia ni Pastor David Jnr Oyedepo na Mkewe Femi Oyedepo

Askofu David Oyedepo ni mtumishi wa Mungu na kiongozi mkuu wa kanisa la Living Faith Church maarufu kama Winners Chapel,kwa sasa Winners Chapel ndio kanisa kutoka Afrika lenye matawi mengi yaliyosambaa duniani kote. Ili kusambaa duniani kote, Bishop Oyedepo aliazimia kila mji mkuu wa nchi yeyote Duniani kuwa na Tawi la kanisa hilo na Mpaka sasa kwa kiasi kikubwa kampeni hii limefanikiwa katika hilo.

Askofu Oyedepo na mkewe Pastor Faith Oyedepo wamejaliwa kuwa na watoto wanne ambao kati yao wawili ni wakiume na wawili ni wa kike.Mtoto wao wa Kwanza ni David Jnr ambaye ni Mchungaji wa kanisa hilo jijini London Uingereza.David Jr alifunga ndoa mwaka 2008 na kwa sasa amejaliwa kupata watoto wawili wa kike na wa kiume.

Pastor David Jnr Oyedepo

Mtoto wao wa Pili ni Mch Isaack Oyedepo, Isaack  kwa sasa ni mchungaji wa Kanisa hilo jijini New York Marekani,David na Isaack Oyedepo kwa pamoja waliwekwa wakfu kama full Time ministers wa kanisa hilo mwaka 2007 na mtumishi wa Mungu Kenneth Copeland. Pastor Isaack alifunga ndoa December 2010 na mpaka sasa wamebarikiwa kupata mtoto wa kiume.

Love Oyedepo ni binti wa kwanza wa Bishop Oyedepo na mtoto wa tatu katika familia hiyo ya kitumishi,Love na yeye pia yupo katika huduma na amekuwa akiambatana na mama yake katika safari za kitumishi.Precious(Joycee) Oyedepo ni Binti wa pili wa Askofu Oyedepo na kitinda mimba wa Familia hiyo.Kwa sasa Precious yuko masomoni barani ulaya.

Pastor Isaack Oyedepo

Kwa mtumishi yeyote au kwa mtu aliyeokoka  kuwa na familia yenye muelekeo wa kitumishi kama huu ni Neema ya ajabu, mara nyingi hususani pale ambapo Mchungaji ana hali mbaya kiuchumi hata watoto huuchukia utumishi, na hata kama mtumishi ana hali nzuri kiuchumi, watoto wanaweza kuwa hawana mzigo na utumishi.Kikubwa hapa tunajifunza kumtegemea Mungu ili atuokoe sisi pamoja na NYUMBA zetu.

1 comment:

  1. PASTOR DAVID AND PASTOR ISAAC,U ARE MY FATHERS AND I WANT U TO KNOW THAT I LOVE U SO MUCH

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...