Wednesday, April 4, 2012

Kutana na Adolph Robert Nzwalla


 Adolph Robert Nzwalla ni Kijana wa Kwanza kwenye Familia ya Marehemu Bishop Robert Nzwalla na Bishop Irene Nzwalla  kutoka katika kanisala Hosanna Christian Centre la jijini Mwanza. Addo kama ajulikanavyo na wengi , anao wadogo zake wapatao wanne ambao ni Priscilla na Gladyce hawa ni mapacha na mdogo wao wa Mwisho   anaitwa Joseph Robert Nzwalla.

Adolph Robert Nzwalla akipiga Keyboard wakati wa Ziara ya John Lisu jijini Mwanza

Adolph Nzwalla ni Mtangazaji  wa redio ya kikristo ijulikanayo kama  HHC Alive Fm yenye makazi yake maeneo ya Kirumba jijini Mwanza inayorusha matangazo yake kupitia  masafa ya 91.9 Fm.Tofauti na utangazaji Addo pia ni Music Director wa Hosanna Praise team ya Jijini Mwanza .Kwa muda mrefu sasa maekuwa akijishughulisha na muziki wa injili akiwa kama muimbaji,mpigaji na mshauri kwa makundi na matukio mbalimbali yafanyikayo jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla.

Slim B    

           Adolph Nzwalla alianza rasmi kujishughulisha na muziki akiwa  mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Nyanza na baada ya hapo alijiunga na shule ya sekondari Mwanza( Mwanza Sec).Baada ya kumaliza Mwanza Secondari Addo alipata nafasi ya Kwenda kusoma Nchini Marekani katika Chuo cha Word of Life School of Ministry ambacho kiko katika Jimbo la Delaware na baada ya kumaliza masomoalirejea Nyumbani na kuunda kundi la Hosanna Praise Team ambalo ndilo anafanya nalo kazi sasa Kama Music Director na Worship Leader wa Group.

             Mwaka 2009 Addo alikuwa ni mmoja wa majaji  katika shindalo la Kusaka Vipaji kwa kanda ya Ziwa lijulikanalo kama“Zaburi Gospel Star Search” ambalo lilikuwa likirushwa na kituo cha Television cha Star Tv cha jijini Mwanza.Mwaka jana Addo alikuwa miongoni mwa watumishi walio-organise ujio wa New Life Band katika jiji la Mwanza. Katika ujio huo kulifanyika Tamasha kubwa la kihistoria katika viwanja vya Furahisha lililohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza pamoja na mama Diana Mwakasege kutoka Arusha. 

Adolph Nzwalla akirun show ya Cross Rythm ndani ya Alive Fm

Addo anauwezo mkubwa wa kupiga Gitaa la solo,Keyboard,drumz na tumba, lakini kwa muda mwingi huonekana akipiga keyboard.katika Huduma hii ya Uimbaji amefanya Huduma na Waimbaji wakubwa kama Jackson Benty,John Lisu,Miriam Lukindo,Pastor David Yared pamoja na waimbaji wengi wa sifa na kuabudu.Katika jiji la Mwanza Addo amekua akiandaa  na wakati mwingine kushirikishwa katika kuandaa matamasha mbalimbali ya kusifu na kuabu.

Adolph Nzwalla akiongoza worship pamoja na mtumishi Ihano Nestory wakati wa ThanksGiving Concert

Hosanna Inc ilibahatika kumuuliza Adolph Nzwalla Maswali kadhaa na alijibu kama ifuatavyo.


Hosanna Inc: Addo ni Concert gani ya Gospel iliyofanyika Mwanza ambayo unaikimbuka sana maishani mwako?

Addo: Nakumbuka nikiwa mmoja wa waandaaji wa Matamasha ya Injili nilipata kufanya kazi na Mwanadada aitwaye Flora Lauwo, au Maarufu kama Flora saloon katika tamasha ambalo lilikuwa ni la kuchangia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hapa Jijini Mwanza. Tangu nimeanza kuhudhuria Matamasha ya Gospel hapa jijini Mwanza hakuna Tamasha limeweza kufikia kiwango kile, watu waliingia katika Uwanja wa CCM Kirumba wakati mvua ilikuwa ikinyesha sana.Kaka huwezi amini mvua ilikuwa inapiga lakini watu bado walikuwa wamepanga Foleni ili kuingia uwanjani.

Nakumbuka tulizunguka Makanisani jumapili ya Tamasha kuwahamasisha watu, kama vile haitoshi  pia tulifanya ROAD SHOWs na waimbaji waliokuwepo ambao ni Dada Rose Muhando,Born Again Squad toka Uganda na Dada Beatrice Muhone, kiukweli Tamasha kama hilo sijawahi kuona tena watu kama hao maana Ilikuwa Gospel Fiesta always i will remember that Concert Bro.

Adolph Nzwalla kulia akiteta jambo na Swahiba Samuel Batenzi(Dube), wakati wa mazoezi ya kujiandaa na ThanksGiving Concert jijini Mwanza.

Hosanna Inc: Kaka tumalizie,hivi ni kwa nini 80% ya concerts za Gospel zinazofanyika uwanja wa CCM Kirumba huwa zinaboa?

Addo: Concert za CCM Kirumba zinaboa coz unakuwa umeenda kuburudika na sio Ibadani,kwa kuwa  kama Matamasha mengine ambayo huwa yanafanyiwa ndani, watu wote huwa tunajumuika katika Ibada lakini matamsha ya playback hakuna Ibada hapo bali ni Kutumbuizwa.

Adolph akiwa na mama yeke mama Askofu Irene Nzwalla(katikati), kushoto ni mama Askofu  Eugine Murisa siku ya Jehova Yu Hai Tour katika ukumbi wa Gold Crest jijini Mwanza.Nyimbo ya Tenzi aipendayo
Yupo Mfariji

His Favourite Bible Verse
Yohana 19:26 Kwa Mungu Yote Yanawezekana,

His Favourite Colour
Purple and Red

Wanamuziki anaowahusudu kutoka Tanzania
John Lisu na Jackson Bent

Wanamuziki anaowahusudu nje ya Tanzania
Benjamin Dube na Donnie MclukinNo comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...