Kiti namba 666 katika Bunge la Ulaya chazua Balaa
Bunge la ulaya ambalo ndani yake kiti chenye namba 666 kiko
wazi
|
Jengo kubwa la mnara wa Ajabu
duniani unaosadikika kuwa mnara mwingine baada ya ule wa Baberi linalotumiwa na
Bunge la Ulaya lililopo Brussels ubergiji, kwa muda mrefu sasa kiti namba 666
kati ya viti 778 vya wabunge wote wa bunge hilo hakina jina la mtu anayekikalia.Katika
viti vyote 778 nina majina majina ya watu wanaovikalia.Mpango wa viti hivyo
nadhifu uko nusu duara na viti vinavyokizunguka kti hicho na majina ya wanao
vikalia ni kama ifuatavyo
663 Montfort
665Thomas Mauro
666 .............
667 Cappato
668 Turco
Katika mlango mkubwa wa kuingilia
katika jengo hilo kuna sanamu kubwa ya mwanamke aliyepanda farasi akiwa nusu
uchi.Uwazi wa kiti hicho umezua maswali mengi hasa kwa wachambuzi wa Biblia
kutokana na Biblia kutamka wazi katika UFUNUO 13 kuwa namna 666 ni ya mpinga
kristo.Wachambuzi wa Biblia wanasema umoja wa ulaya ni moja kati ya maeneo
ambayo yanaharakisha ujio wa mpinga kristo.
Viongozi
wa serikali na Dini wajadili Amani Tanzania
Viongozi wa serikali, dini, na
taasisi mbalimbali nchini wiki iliyopita wamekutana kwa siku mbili ili kujadili
mambo mbalimbali yatakayodumisha AMANI na Umoja wa watanzania.Mkutano huo
ulifanyika katika Hotel ya White Sands ya jijini Dar es salaam na kufunguliwa
na Makamu wa Rais Mh Mohamed Gharib Bilal ambaye aliwaasa viongozi wa didi kuwa
mstari wa mbele katika kuhimiza na kulinda umoja wan kitaifa na kusaidiana
katika kukemea vitendo vya kifisadi.
Kwa mujibu wa Askofu mkuu wa kanisa
la Tanzania Assemblies of GOD(TAG) Askofu Barnabas Mtokambali ambaye alihudhuria
kikao hicho alisema “ kikao hiki kimejenga msingi wa utatuzi wa matatizo ambayo
yanaweza kuondoa Amani ya nchi yetu”
Mawaziri
waonywa Ikimbieni hukumu ya Mungu
Mawaziri wenye tuhuma mbalimbali
zinazowagusa wao binafsi au kushindwa kutekeleza wajibu wao na kusababisha
uchungu na mateso makali kwa watu masikini na wale wenye kipato cha chini huku
kukiwa na tishio la kutoweka kwa amani kutokana na kukithiri kwa tuhuma za
ufdisadi na rushwa.
Wito huo umetolewa na viongozi wa
dini na wabunge mbalimbali waliohojiwa na gazeti la jibu la Maisha katika
nyakati tofauti tofauti.Akiongea kwa kujiamini Mbunge wa Iringa mjini Piter
Msigwa alisema kuwa yeye alishiriki katika kamati ya bunge iliyokuwa
ikichunguza tuhuma zilizokuwa zinamkabili waziri wa maliasili na utalii Mh
Ezekiel Maige na alioyaona huko yanatisha kwa kuwa Mungu huwa na tabia ya
kuchoka na kushusha hukumu yake kwa muhusika.
Msigwa ambaye pia ni Mchungaji
alisema, nchi haiko salama kuliko unavyodhani, kwa kuwa kuna watu wengi
walipaswa kufanya jambo kuliokoa taifa lakini bado hawajafanya. Wakati umefika
kwa viongozi wa dini kujitenga na pesa zinazoletwa makanisani na watuhumiwa wa
Ufisadi na tuwe makini kama nabii Mika kwa kuwaambia hapana.
Alisema kama viongozi wa dini
wakisimama wakakataa wanasiasa mafisadi wanaojaribu kukimbilia kanisani
kujisafisha kwa fedha chafu, wanachi hao wakisimama imara na kusema wizi, basi
na wanasiasa wema waliosalia wakavunja nira na mafisadi
nchi itasalimika.
Kutoka
gazeti la Msemakweli
Pope Benedict |
Mkuu
wa wakatoriki duniani atangaza maisha yake kufikia ukingoni
Kiongozi wa kanisa katoriki duniani
Papa Benedict XVI amesema kwamba hivi sasa anakaribia mwisho wa maisha yake
katika umri wa miaka 85 alionao, lakini anauhakika kwamba Mungu atamsaidia katika
kufanya kazi zake za Kitume.Kauli hiyo isiyotarajiwa imetolewa na kiongozi huyo
wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa jijini Vatiokani nchini ITALIA yalipo makao
makuu ya kanisa hilo duniani.
VCC
Pastors fellowship kuandaa mkutano mkubwa jijini Dar es salaam
Huduma ya Pastors Fellowship
inayoongozwa na kanisa la Victory Christian Centre lililo chini ya Mch Huruma Nkone,
limefanikiwa kutimiza maono yake baada ya kukusanya wachungaji mia tano wa
mikoa ya Pwani na Dar es salaam.Ushirika huo wa wachungaji ulikutana katika
ukumbi wa Hotel ya Landmark ya jijini Dar es salaam na moja kati ya mikakati
yake ni kuandaa mkutano mkubwa utakaofanyika katika viwanja vya Jangwani mnamo
mwezi sita mwaka huu wa 2012.
Gazeti la Nyakati
Mchungaji
Masanja asema wanaoruhusu wanawake kuvaa suruari kanisani wamepotoka
Mchungaji Gervas Masanja wa kanisa
la Pentekoste Mission Church la nchini Tanzania akiongea na Gazeti la Nyakati
baada ya kuulizwa kama kuna tatizo lolote la kimaadili kwa mwanamke mkristo
kuvaa suruali ibadani,Mch Masanja alijibu kama ifuatavyo “Kuvaa suruali kwa
Mwanamke ni dhambi, Mapokeo na utandawazi vimewapoteza wengi, watumishi
wanaowaruhusu waumini wao kuvaa suruali haijalishi ni kanisani au popote, hao
sio watumishi wa Mungu mtu awe tayari kuwa na Bwana wakati wote.
Wasabato
masalia wataka waombwe radhi
Wachungaji watatu waliojitenga na
kanisa la sabato(SDA) na kuanzisha kanisa linalojulikana kama Seventh Day
Reformed Remnants maarufu kama Wasabato
Masalia wameutaka uongozi wa kanisa la SDA kuwaomba radhi vinginevyo
watawapleka mahakamani..Hatua hii imekuja baada ya Kanisa la SDA kuwafungukia
mashitaka viongozi wa masalia kwamba wamedurufu vitabu vya mwanzilishi wa
kanisa la SDA Nabii Ellen White pasipo idhini ya Nabii