|
Kiongozi Wa Maimamu Zanzibar,Farid
Hadi Ahmed
|
Kila
sifa njema zinamstahikia Allah, Subhanah wa Taala, isofichikakwake dhulma wala
harudishi dua ya mwenye kudhulumiwa. Rehma na amani zimshukie Mtume Muhmmad
(s.a.w) kipenzi chake na cha umma, mtetezi wa waliodhulimiwa hata kabla ya
kupewa Utume.Mhishimiwa
Rais,Kwa mapenzi makubwa, baada ya kuisoma kwa utulivu khutuba yako ya siku
tukufu ya Iddil Alfitri, nimelazimika kuandika barua hii kufuatana na kauli
mbiu ya Mtume Muhammad (s.a.w) inayosema:
“…Dini ni
nasaha…nasaha kwa Allah (S.w.T) na ni nasaha kwa Mtume (s.a.w.) na kwa viongozi
wa Waislamu na kwa watu wote…”
Mh.
Rais;
Ni
kweli nchi yeti ya Zanzibar imechafuliwa jina lake kuwa ni nchi ya amani kama
ilivyogeuzwa nchi yetu na ndugu zetu na kufanywa kuwa ni koloni lao baada ya
mkoloni Mwingereza kutupa uhuru mwaka 1963 na kuwa na kiti chetu Umoja wa
Mataifa huku walimwengu wote wakishuhudia; kiti ambacho kwa uwezo wake Allah
atakirejesha karibuni na wewe ukiwa rais wa Zanzibar au uliyemwakilisha kuweza
kuketi juu yake Insha’allah na sisi wananchi wako wa Zanzibar tukifurahikia
jambo hilo adhimu.
Mh.Rais;
Ni
kweli nchi yetu inatiwa dosari lakini si kweli kuwa wananchi wa Zanzibar ndio
wanaosababisha dosari hiyo na doa hilo la uvunjifu wa amani; ushahidi wa maneno
haya tutaupata tukirejea na kutizama kwa jicho la uadilifu na insafu katika
matukio tafauti. Kwa hakika tukifanya hivyo tutagundua bila ya taabu kuwa Jeshi
la Polisi la Tanzania ndio wahusika wakuu na waanzilishi wa vurugu na uvunjifu
wa amani ya nchi yetu ya Zanzibar kwa mara zote tatu, nikimaanisha machafuko
yaliyotokea tarehe 25-26/5/2012 mjini Zanzibar na yale ya kuhujumu waumini na
kunajisi misiskiti tarehe 17/6/2012, Donge, Mahonda na Mkokotoni pamoja na
hujuma ya tarehe 20/7/2012 msikitin pia dhidi ya Waislamu walokusanyika msikiti
wa Mbuyuni kuwasalia ndugu zao waliofariki kwa ajali ya meli ya Mv. Skaget.
Waislamu tulihujumiwa ndani ya msikiti.
Jeshi
la polisi halikusita hapo bali liliwaingilia wananchi wanyonge mpaka
ndani ya nyumba zao na kuwatendea matendo haramiya ya chuki na uhuni na katika
waliotendewa matendo hayo maovu walikuwa wanawake na watoto wachanga. Polisi
hao wakhalifu wa sharia waharibifu wa amani walifika hadi ya kutupa mabomu ya
madawa makali ndani ya majumba ya raia bila ya kujali athari zitakazowasibu
watoto wachanga na wanawake wenye kunyonyesha.Iwapo jeshi la polisi lililopewa
jukumu la kulinda sharia, kuweka amani na kuwahami wananchi na mali zao ndio
wenye kuvunja shariakwa kuwahujumu watu bila ya
sababu,
wananchi na haki zao zitalindwa na nani?
Mh.Rais;
Matokeo
ya ukiukwaji wa sharia na haki za binadamu yaliyopelekea kuiharibia nchi yetu
ya Zanzibar sifa yake ya amani na utulivu yamesababishwa na jeshi la polisi la
Tanzania lililoacha kutekeleza wajibu wake wa kutunza amani ya nchi yetu
Zanzibar . La kusikitisha zaidi ni kuwepo baadhi ya watendaji wako wa karibu
wanaopotosha ukweli na kuifanyia khiyana nchi yetu ya Zanzibar kwa kufikisha
kwako taarifa za uongo zilizopelekea kuitia doa na kuiharibu khutuba yako
ilojaa maneno matukufu ya Allah Subhanah wa Taala pamoja na mafunzo kutoka
Sunna za Mtume (s.a.w), khutuba ambayo ilitarajiwa kukemea dhulma za jeshi
la polisi dhidi ya Waiislam na nyumba tukufu za Allah (S.w.T) iliyohujumiwa
pamoja na wanawake na watoto wachanga ndani ya majumba kama ulivotetea makanisa
na kubainisha hatari na ubaya wa walioyachoma makanisa hayo kwa lengo la kutaka
kuanzisha fitna baina ya Waislam na jirani zao Wakristo waliokaribishwa nchini
Zanzibar na kuishi pamoja nao miaka mingi kwa amani kiasi ambacho haijawahi
kutokea Muislamu kulitusi kanisa licha kulichoma moto, kwani hayo ni kinyume na
mafunzo
ya
dini yetu tukufu ya Kiislamu.
Mh.Rais; Watu wanaokuwa karibu na Rais ni watu
muhimu sana katika kufanikisha dhana ya uadilifu na utawala bora na wa haki
usioogopa kukemea maovu hata kama walotenda au kuteleza ni Jeshi la Polisi
kwani pia wao ni binaadamu siajabu kutenda makosa kwa maksudi seuze
kuteleza, Allah Sbhanah wa Taala anatwambia: “…Enyi mloamini kuweni wasimamizi
wa Allah wenye kushuhudia ukweli hata kama ni dhidi ya nafsi zenu…” Kwa hivyo,
kosa kubwa zaidi ni kuuficha ukweli au kumpotosha kiongozi wa nchi hadi kufikia
kuwashushia sifa wasiostahiki, wahuni ambao waliwatendea ya uhuni na dhulma
kubwa hata wanawake na watoto.
Ni
khatari wadhulumiwa wanapofikishwa kumshtakia Mfalme wa Mbingu na Ardhi juu ya
dhulma wanazotendewa. Isitoshe, khiyana ya watu kamaa hao wa karibu na viongozi
kila inapojikariri khiyana hiyo inajenga hisiya kwa wenyeji wa nchi hii ambao
wengi wao ni Waislamu kuwa wanabaguliwa, na sio wao tu bali hata
kudharauliwa nyumba zao tukufu za ibada na kuthaminiwa makanisa peke yake. Sisi
Waislamu hatutaki nyumba zozote za ibada zidharauliwe.Nyumba zote za ibada
lazima ziwekewe hishima zinazostahiki.
Mh.Rais;
Kwa
heshma zote naomba zichunguzwe sana sifa mbili kwa watu wote wa karibu na
viongozi, sifa mbazo ni hatari kuzikosa tena zinaweza kuiangamiza nchi yetu
tukufu ya Zanzibar . Sifa hizo si nyengine illa ni ukweli na uaminifu
ambazo ni kinyume na uwongo na khiyana.
Yarabbi
Muumba Mbingu na Ardhi, usieshindwa na jambo, tunakuomba muhifadhi Rais wetu,
turejeshee nchi yetu kwa salama na amani, DOLA HURU YA ZANZIBAR, wastiri
wanawake na watoto wachanga majumbani na Wazanzibari wote tunaodhulumiwa kwa
kudai uhuru wa nchi yetu ya
Zanzibar
uloporwa na jirani zetu, ndugu zetu baada ya kutoka kwa wakoloni.
Amir
Mkuu,
Jumuiya
ya Maimamu Zanzibar
Farid
Hadi Ahmed
Source: Chediel Charles wa Rundugai